– Protus Momanyi mwenye umri wa miaka 87 aliaga dunia baada ya kuugua kisukari kwa muda mrefu
– Aliwahi kuwa mbunge mara mbili wa eneo la Bonchari kando na kuteuliwa kama Waziri wa Utalii na Wanyamapori enzi za marehemu rais mtaafu Daniel Moi
– Amewaacha mke Teresia Moraa na watoto wanne
Familia ya aliyekuwa mbunge wa Bonchari Protus Momanyi inaomboleza kifo chake kilichotokea Jumapili, Julai 5 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Hadi kifo chake Dkt Momanyi ambaye alikuwa na umri wa miaka 87 alikuwa akipokea matibabu katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta baada ya kuugua kisukari The Standard iliripoti.
Protus Momanyi aliaga dunia baada ya kuugua kisukari kwa muda mrefu kulingana na familia yake. Picha: The Standard. Source: UGC
Marehemu alishinda uchaguzi katika eneo bunge hilo mara mbili kando na kuhudumu kama Waziri wa Utalii na Wanyamapori wakati wa utawala wa marehemu rais mstaafu Daniel Moi.
Alipojitosa katika ulingo wa siasa, aliwania kiti cha ubunge cha eneo la Wanjare linalofahamika kwa sasa kama Mugirango Kusini mnamo 1969 lakini alishindwa.
Marehemu amewaacha mke Teresia Moraa na watoto wanne.
Kwa sasa familia yake inaomba msaada kutoka kwa wahisani ili kumpa mazishi ya heshima baada ya kuishiwa na hela walizokuwa nazo kugharamia matibabu yake hospitalini.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.