Connect with us

General News

Wekeni akiba muachane na hongo, Matiang’i aambia polisi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wekeni akiba muachane na hongo, Matiang’i aambia polisi – Taifa Leo

Wekeni akiba muachane na hongo, Matiang’i aambia polisi

NA WINNIE ONYANDO

WAZIRI wa Usalama wa Ndani, Fred Matiang’i amewahimiza maafisa wa polisi ku – jiunga na vyama mbali mbali vya akiba na mkopo ili wakome kuitisha hongo ndogo ndogo na makosa mengine.

Akizungumza jana katika mkutano wa kila mwaka wa chama cha ushirika cha polisi nchini, Dkt Matiang’i alisema kuwa wakiweka akiba basi watakoma kuhusika katika makosa ya kushirikiana na majambazi na hata kuwakodisha bunduki.

“Ninahimiza kila afisa wa polisi ajiunge na chama cha ushirika cha akiba na mkopo kuwekeza pesa ili tukomeshe makosa yanayoweza kuepukika. Hatutaki kusikia kila mara kuwa polisi fulani alishirikiana na majambazi na kuwauzia bunduki. Ukiweka akiba, basi maisha yako na ya familia yako yatakuwa sawa,” akasema Dkt Matiang’i.

“Ukianza kuweka akiba saa hii, basi katika kipindi cha mwaka mmoja, utapata kuwa umepiga hatua kubwa sana,” akasema Dkt Matiang’i.

Aliwataka maafisa hao wa usalama pia wajenge nyumba zao ili waondoe aibu ya kuchangiwa pesa baada ya kustaafu.

“Tungependa kuwa kila mmoja baada ya kustaafu, awe ana nyumba nzuri na ametunza familia yake. Weka pesa zitakazokusaidia ukiwa mzee ukipumzika nyumbani.

Hatutaki kusikia afisa wa polisi anachangi – wa pesa ilhali alikuwa akipokea mshahara kila mwezi.” Kando na kutoa mafunzo yanayohusiana na kazi kwa maafisa wa usalama, Dkt Mat – iang’i alitoa wito kwa serikali pia iwafunze namna ya kuweka akiba kwa maisha ya baadaye.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending