Connect with us

General News

Wetang’ula asuta Raila kuhusu ahadi za kufufua viwanda vya sukari – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wetang’ula asuta Raila kuhusu ahadi za kufufua viwanda vya sukari – Taifa Leo

Wetang’ula asuta Raila kuhusu ahadi za kufufua viwanda vya sukari

NA BRIAN OJAMAA

KINARA wa Muungano wa Kenya Kwanza Moses Wetang’ula, amemkashifu mgombea wa urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga, kuhusiana na ahadi za kufufua viwanda vya sukari katika eneo la Magharibi mwa Kenya.

Seneta huyo alimlaumu Bw Odinga kwa masaibu ya kifedha yanayokumba Kiwanda cha Sukari cha Mumias.

“Nilimsikia Bw Raila alipokuwa akifanya kampeni katika maeneo ya Magharibi mnamo wikendi, akisema kuwa atakapoingia mamlakani, atafufua viwanda vyetu vya sukari. Huo ni upuzi mtupu, acha uongo kwenye kampeni, viwanda vingi vya sukari vimekwama,” alisema Bw Wetang’ula akiwa katika kijiji chake cha Namuyemba, eneo la Kanduyi, Kaunti ya Bungoma.

Alifichua kuwa jina la Bw Odinga limetajwa mno kuhusiana na kusambaratika kwa kampuni hiyo na hawezi kutoa suluhisho kwa matatizo yanayokabili sekta ya sukari.

“Hatuwezi tukasuluhisha matatizo katika sekta ya sukari kupitia mbinu zilezile za kuyafufua. Umekuwa sehemu ya matatizo yaliyowagharimu wakazi,” alisema.

Huku akitaja ahadi zilizotolewa na kiongozi wa ODM kuhusu kufufua sekta ya sukari kama feki, Seneta huyo wa Bungoma alisema, Kenya Kwanza ina ajenda zitakazosaidia kuanzisha oparesheni za viwanda hivyo mara tu itakapochaguliwa mamlakani.

“Tuna manifesto ya kufufua uchumi tutakayoanzisha baada ya kutwaa mamlaka katika uchaguzi wa Agosti 9, 2022, tunahitaji kuwaeleza watu wetu ukweli wala si uongo ili tupate kura zao,” alisema.

Akifanya kampeni katika eneo la Shinyalu Kaunti ya Kakamega, Bw Odinga aliahidi kupatia kipaumbele ufufuzi wa viwanda vya sukari ikiwa atachaguliwa mamlakani.

Alitaja kampuni ya Mumias na Sony kama baadhi ya viwanda vya sukari atakavyofufua ili kuunda nafasi za ajira na kuboresha ukuaji wa uchumi eneo hilo.

“Mara nitakapoingia mamlakani nitafufua viwanda vya sukari ambavyo vipo taabani ili kuimarisha wakulima kuvuna kutokana na jasho lao,” alisema.