[ad_1]
Wijnaldum afungua akaunti ya mabao kambini mwa PSG waliokabwa koo na RB Leipzig katika UEFA
Na MASHIRIKA
KIUNGO wa zamani wa Liverpool, Georginio Wijnaldum, alifunga bao lake la kwanza ndani ya jezi za Paris Saint-Germain (PSG) katika mchuano wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) uliowakutanisha na RB Leipzig mnamo Jumatano usiku nchini Ujerumani.
Wenyeji Leipzig waliwekwa uongozini na Christopher Nkunku katika dakika ya nane kabla ya Wijnaldum ambaye ni raia wa Uholanzi kusawazisha mambo kwa upande wa PSG katika dakika ya 21.
Bao hilo liliwapa masogora wa kocha Mauricio Pochettino motisha zaidi na wakafunga wenyeji wao bao la pili kupitia kwa Wijnaldum. Hiyo ilikuwa baada ya Leipzig kupoteza penalti iliyochwanjwa na fowadi mzoefu, Andre Silva.
Dominik Szoboszlai alisawazishia Leipzig mwishoni mwa kipindi cha pili kupitia penalti. Mkwaju huo ulitokana na tukio la beki Presnel Kimpembe kumkabili Nkunku visivyo ndani ya kijisanduku sekunde chache kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa mechi kupulizwa.
PSG ambao ni miamba wa soka ya Ufaransa walitandaza mchuano huo dhidi ya Leipzig bila kujivunia maarifa ya fowadi matata raia wa Argentina, Lionel Messi, aliyepata jeraha katika mechi ya awali ya Ligi Kuu (Ligue 1) iliyoshuhudia waajiri wake wakipepeta mabingwa watetezi Lille 2-1 ugani Parc des Princes.
Sare iliyosajiliwa na PSG dhidi ya Leipzig iliwateremsha hadi nafasi ya pili kwenye Kundi A kwa alama nane, moja nyuma ya viongozi Manchester City waliocharaza Club Bruges ya Ubelgiji 4-1 uwanjani Etihad. Leipzig kwa sasa wanakamata nafasi ya tatu kwa pointi nne, tatu zaidi kuliko Club Bruges.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
Next article
Ruto aahidi yaliyoshinda UhuRuto
[ad_2]
Source link