Connect with us

General News

Wine Bobi Wine sasa amshambulia Museveni kwa muziki – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wine Bobi Wine sasa amshambulia Museveni kwa muziki – Taifa Leo

Wine Bobi Wine sasa amshambulia Museveni kwa muziki

Na DAILY MONITOR

KIONGOZI wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu, almaarufu Bobi Wine, sasa ameamua kutumia muziki kumshambulia Rais Yoweri Museveni.

Wine jana alizindua video ya wimbo mpya kwa jina la ‘Ogenda’; neno la Kiganda linalomaanisha ‘Utaanguka’.

Kulingana na Wine, wimbo huo unamlenga Rais Yoweri Museveni moja akimshutumu kwa kukiuka ahadi yake ya kuleta demokrasia nchini humo.

Wine aliambia wanahabari kuwa alitumia picha za kutisha kwenye wimbo huo kuashiria utawala wa Rais Museveni anaodai kwamba unatisha.

“Utawala nchini Uganda umewekeza pesa nyingi kuficha ukatili na dhuluma ambazo imekuwa ikitekeleza,” alisema.

Bobi Wine alisema vyombo vya habari nchini Uganda vimezimwa na njia pekee ya kufichua uozo huo ni kupitia muziki.

“Haki inaweza kupatikana pale tu tunapofichua uhalifu, ndiyo maana tunaendelea kuuibua, hiyo ndiyo njia pekee tunayoweza kupambana nayo,” alisema.