Connect with us

General News

Wito serikali ilinde utalii usiporomoke tena – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wito serikali ilinde utalii usiporomoke tena – Taifa Leo

Wito serikali ilinde utalii usiporomoke tena

Na WINNIE ATIENO

WADAU wa sekta ya Utalii eneo la Pwani wameitaka serikali ya kitaifa ikabiliane na changamoto za ugaidi ili kuilinda na athari zake.

“Habari yoyote mbaya hasa inayohusu mauaji si njema kwa sekta ya utalii. Lamu ni kaunti kubwa sana ambapo mtu mgeni hawezi kuelewa ukisema Lamu kisiwani au kwingineko. Hakujawahi kutokea shambulio lolote la kigaidi kisiwani au hata katika maeneo ya kitalii,” alisema Mkurugenzi wa Pollman, Bw Mohammed Hersi.

Wawekezaji wa utalii wakiongozwa na afisa mkuu mtendaji wa Muungano wa Utalii wa Pwani ya Kenya, Bw Julius Owino, na afisa mkuu mtendaji wa chama cha wahudumu wa hoteli nchini Kenya Dkt Sam Ikwaye waliitaka serikali kuimarisha usalama.Walisema watalii wanapenda kuzuru maeneo salama.

Hata hivyo, wakazi na viongozi wa Lamu walitakiwa kushirikiana na idara ya usalama kupasha idara ya usalama kuhusu utovu wa usalama.

Mtaalamu huyo wa utalii aliwataka wenyeji kutekeleza jukumu lao kuripoti mgeni yeyote wanayeshuku ili kuzuia mashambulizi.

“Mauaji hayafai. Hali ya Lamu itatuathiri moja kwa moja, tunaisihi serikali kuimarisha misako,” alisema Bw Hersi.

Naye Bw Owino alisema shambulizi hilo lilifanyika sehemu ambayo watalii hawazuru. Aliisihi idara ya usalama kukabiliana na jinamizi hilo.

“Hakikisheni Kenya iko salama. Tumetoka katika kipindi kizuri sana cha utalii Disemba mwaka jana ambapo sekta ilinoga, tunaomba utulivu uendelee kushuhudiwa ili biashara zetu zinoge,” alisema Bw Owino.

Aliwahakikishia watalii kuwa serikali inashughulikia suala hilo.Dk Ikwaye alisema shambulio hilo lilitokea wakati wawekezaji wa utalii wakijiandaa kwa msimu wa Aprili.

“Kwa sasa, tunafanya vizuri sana hadi Aprili ambapo msimu wa utalii utapigwa jeki zaidi kutokana na sherehe za Pasaka.”

“Kwa sasa tunavuna kutoka kwa mikutano kwa sababu watalii wa kimataifa wamedorora biashara za kimataifa bado iko chini,” alisema Dk Ikwaye.

Dkt Ikwaye alisema mashambulizi hayo si mazuri kwa sekta ya utalii.

“Hasa kwa kuwa tumekuwa na kipindi cha utulivu. Lakini wakazi wa Lamu wanapaswa kutekeleza wajibu wao katika kusaidia vyombo yya usalama kwa kutoa habari. Viongozi pia wanapaswa kusaidia vita dhidi ya ugaidi. Ni jambo la kimataifa, linahitaji umakini zaidi,” aliongeza Dkt Ikwaye.

Lamu ambayo inapakana na Somalia, hemaya ya kundi la kigaidi la Alshabaab. Mara kadhaa Lamu imekumbwa na mashambulizi ya kigaidi.

Kaunti hiyo imekuwa kwenye rada za kimataifa huku baadhi ya nchi za Ulaya na Uingereza zikiwaonya raia wake dhidi ya kuzuru baadhi ya maeneo ya Lamu kutokana na ukosefu wa usalama.

Katika mahojiano ya awali, Waziri wa Utalii na Wanyamapori Bw Najib Balala alilaani nchi ambazo zimekuwa zikiwaonya raia wake dhidi ya kuzuru baadhi ya maeneo ya Afrika kutokana na vitisho vya ugaidi.

Alisema nchi za kigeni zimekuwa zikitoa ushauri na vikwazo kwa nchi za Afrika kwa njia zisizo za haki.