Connect with us

General News

Wito uteuzi wa Kidato cha Kwanza uwe wa uwazi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wito uteuzi wa Kidato cha Kwanza uwe wa uwazi – Taifa Leo

Wito uteuzi wa Kidato cha Kwanza uwe wa uwazi

NA LAWRENCE ONGARO

WITO umetolewa uteuzi wa wanafunzi kuingia Kidato cha Kwanza ufanywe kwa uwazi bila mapendeleo yoyote.

Mbunge wa Thika Bw Patrick ‘ Jungle’ Wainaina, alidai wanafunzi wengi kutoka eneo la kati hawanufaiki na kusajiliwa katika shule za kitaifa.

Alieleza wengi ambao wananufaika ni wale wametoka maeneo mengine.

“Ni muhimu hata wanafunzi kutoka maeneo ya Thika na hata Kiambu kwa jumla wapewe nafasi kujivunia shule za kitaifa kwani wazazi wao walichangia pakubwa wakati zilikuwa zikijengwa,” alifafanua mbunge huyo.

Alisema kwa muda wa miaka mitano ambapo amekuwa mbunge, ameweza kukarabati shule za msingi zipatazo 56 huku zikigeuka kuwa na mazingira ya kupendeza.

“Baadhi ya mambo ambayo yametekelezwa ni kuweka matangi ya lita elfu 10,000 kwa kila shule, kurekebisha, milango, madirisha na kuweka waya ya kuzunguka shule hizo kwa lengo la kuthibiti usalama,” alieleza Bw Wainaina.

Alisema ukarabati huo umeleta mabadiliko mengi ya kimasomo huku wanafunzi wengi wakifanya vyema katika masomo yao.

Mwenyekiti wa shule za msingi za kibinafsi mjini Thika Bi Mary Kirika alipongeza serikali kwa kuendeleza mtaala wa CBC.

Alisema mpango huo utaleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu.

Bi Kirika alitaka usajili wa wanafunzi katika shule za kitaifa uwe wa haki bila ubaguzi.

Alisema wanafunzi wengi wanaojiunga na shule za kitaifa katika kaunti ya Kiambu wanatoka maeneo ya mbali jambo alilosema linastahili kuchunguza kwa makini.

Alisema kuwa walimu wanastahili kufunzwa mtaala mpya wa CBC huku akipongeza shule za kibinafsi kwa kuchukua msimamo huo.

Afisa wa elimu katika kaunti ndogo ya Thika Morris Sifuna alisema serikali itafanya kila jambo kuona ya kwamba wanafunzi wanaojiunga na Kidato cha Kwanza wanatendewa haki katika usajili huo.

Aghalabu wazazi wengi hupata matatizo mengi kuwaingiza wana wao katika Kidato cha Kwanza ikitokea kwamba wamekosa nafasi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending