Connect with us

General News

Wito watu wajiunge na vikundi, vyama vya ushirika kupunguza gharama ya juu ya maisha – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wito watu wajiunge na vikundi, vyama vya ushirika kupunguza gharama ya juu ya maisha – Taifa Leo

Wito watu wajiunge na vikundi, vyama vya ushirika kupunguza gharama ya juu ya maisha

NA SAMMY WAWERU

WANANCHI wamehimizwa kujiunga na vyama vya ushirika na pia kubuni miungano ili kusaidiana nyakati hizi ngumu kimaisha na kiuchumi.

Wito huo umetolwa na mwekahazima wa Chama cha Ushirika cha Wahudumu wa Tuktuk na Maruti eneo la Githurai 45, Ruiru, Kaunti ya Kiambu, Bw Dixon Mwangi.

Afisa huyo wa GTM Sacco, amesema ni kupitia ushirikiano wa pamoja, Wakenya wataweza kupunguza gharama ya maisha.

“Chini ya Sacco au miungano, mwanachama anapopatwa na tatizo washirika watamfaa pakubwa kupitia ukusanyaji wa pesa kumkwamua,” Bw Mwangi akasema.

Alisema hayo katika mkutano na wamiliki wa magari, chini ya GTM Sacco.

“Kwa mfano, nina hafla ya kumtolea mke wangu mahari na ninaamini ushirikiano wetu utaifanikisha,” akadokeza.

Walioimarisha vyama vya ushirika na miungano, baadhi kupitia makundi hununua bidhaa za kula kwa bei ya jumla na kugawana wenyewe kwa wenyewe.

Hatua hiyo inawapunguzia gharama ya juu inayotokana na mfumko wa bei ya bidhaa,

Bidhaa za kula kama vile unga, maziwa, sukari, mafuta ya kupika, miongoni mwa nyinginezo zinaendelea kuwa ghali kipindi ambacho nchi na ulimwengu kwa jumla unaendelea kuuguza athari za janga la corona.

Mamia na maelfu walipoteza nafasi za kazi hasa baada ya Kenya kukumbwa na ugonjwa wa Covid-19.

Baadhi walifunga biashara zao, hususan sekta ya utalii inayojumuisha wahudumu wa hoteli, mikahawa, vilabu na baa.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending