Connect with us

General News

Yaya aliyenajisi mtoto asukumwa jela maisha – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Yaya aliyenajisi mtoto asukumwa jela maisha – Taifa Leo

Yaya aliyenajisi mtoto asukumwa jela maisha

NA BRIAN OCHARO

MWANAMKE mmoja amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kunajisi mtoto na kuuza video za unyama huo, baada ya kujitetea kuwa alivutiwa na ahadi za ajira.

Kesi hiyo imefichua jinsi maovu yanatendeka mitandaoni bila wazazi wengi kujua.

Bi Edda Wakesho, aliyekuwa yaya, alipatwa na hatia Jumatatu katika Mahakama ya Mombasa kwa makosa hayo yaliyotendeka kati ya Juni 2020 na Oktoba 2021.

Alipokuwa akijitetea katika kesi hiyo, ilibainika kwamba kuna makundi ya watu katika mitandao ya kijamii ambao hutumia ahadi za pesa, ajira na wakati mwingine kutoa vitisho ili watumiwe picha na video za vitendo vichafu vinavyofanyiwa watoto wadogo.

Wao husambaza picha hizo kupitia kwa mitandao ya intaneti ambapo inashukiwa watumizi huhitajika kulipa ada ili kuziona.

Mhukumiwa huyo alianza kushiriki katika kundi lililo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook muda mfupi baada ya kupokea mshahara wake ambapo alinunua simu ya kidijitali.

Aliambia mahakama kuwa, alianza tabia hiyo baada ya kutangamana na mtu asiyemfahamu aliyejiita Lucracea kwenye Facebook.

Lucracea ndiye alimtambulisha kwa ukurasa wa mtandao huo ambapo washiriki wake walikuwa wanatuma picha za uchi na video za ngono.

Kulingana naye, ahadi za kutafutiwa ajira ili ajiinue kimaisha endapo angetuma picha na video zilimvutia kufanya hivyo.

“Waliniahidi kazi kwa sharti kwamba nirekodi video ya ngono na kuwatumia,” aliambia mahakama.

Wakati wowote alipositasita kutuma picha na video hizo kwa kuona kama faida zinachelewa, anasema alitishiwa maisha.

Kulingana na hati ya mashtaka, Wakesho, 20, alimdhulumu mvulana huyo kingono na kimakusudi na kinyume cha sheria akatoa picha za ngono akifanya makosa hayo na mtoto huyo.

Aliomba msamaha kutoka kwa familia ya mwathiriwa, akisema kwamba alikuwa ametenda makosa hayo kutokana ana tishio kwa maisha yake na kwamba alikuwa amekata uhusiano na kundi hilo.

Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Shanzu, Bi Florence Macharia, alimpa pia kifungo cha miaka kumi kwa kosa la kuhusika na usambazaji wa filamu za ngono ya watoto.

“Mtoto huyo hakujua kilichokuwa kikiendelea. Mshtakiwa atatumikia adhabu hizo mbili kwa wakati mmoja,” hakimu alisema.

Familia ya mvulana huyo ilisema mshukiwa alitekeleza majukumu yake kwa bidii bila wao kutambua kosa lolote hadi alipoondoka kwa kisingizio cha kutafuta kazi aliyosomea ya kushona.

Hata hivyo, familia hiyo imeelezea wasiwasi wao kuwa picha za uchi na video za ngono zinazohusisha mtoto huyo huenda bado ziko kwenye mtandao na kuwataka wapelelezi kuingilia kati.

Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi wa Watoto Pwani, Bw Andrew Warui, alisema kitengo hicho kinachunguza visa sawa na hivyo katika eneo hilo ambapo watoto wadogo wamenyanyaswa kimapenzi na walezi wao na kanda za vitendo hivyo haramu kusambazwa kupitia majukwaa mbalimbali ya mtandao ili kujinufaisha kifedha.

Kitengo hiki pia kinajitahidi kukomesha mitandao ya kimataifa inayoshirikiana na walezi waovu kuendeleza biashara ya ponografia ya wa – toto, kwa mujibu wa Bw Warui.