Connect with us

General News

Zain Manji aibuka mshindi wa Muthaiga Safaricom Golf Tour – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Zain Manji aibuka mshindi wa Muthaiga Safaricom Golf Tour – Taifa Leo

Zain Manji aibuka mshindi wa Muthaiga Safaricom Golf Tour

Na GEOFFREY ANENE

ZAIN Manji ameshinda duru ya tatu ya mashindano ya Safaricom Golf Tour baada ya kuzoa alama 41 uwanjani Muthaiga.

Katika mashindano hayo yaliyovutia zaidi ya wanagofu 200 mnamo Machi 12-13, Manji alivuna alama 19 katika mashimo tisa ya kwanza na alama 22 katika mashimo tisa ya mwisho kufikisha jumla ya alama 41.

“Kupata fursa ya kushiriki duru ya tatu ya Safaricom Golf Tour na kumaliza nambari moja katika uwanja mgumu kunanipa matumaini makubwa katika uchezaji wangu wa gofu. Inafurahisha sana kushindana na wachezaji wazuri,” alisema Manji anayeungana katika fainali kubwa na washindi wa duru mbili za kwanza, kadi wa zamani Cyprian Bundi (Nanyuki) na chipukizi Leo Gitonga (Limuru). Fainali kubwa itaandaliwa Vipingo Ridge mwezi Agosti.

Wakati huo huo, Fuward Abdallah na Lucy Njoroge walitawala vitengo vya wanaume na wanawake kwa alama 39 na 40, mtawalia. Duru ya Muthaiga ilikamilika baadaye jana baada ya chipukizi 250 kupata kushindana na pia mafunzo. Baada ya Muthaiga, wanagofu sasa wataelekea klabu ya gofu ya Nyanza mnamo Machi 26-27.