Connect with us

General News

Zelensky ataja uvamizi wa Urusi kuwa ugaidi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Zelensky ataja uvamizi wa Urusi kuwa ugaidi – Taifa Leo

Zelensky ataja uvamizi wa Urusi kuwa ugaidi

NA MASHIRIKA

KYIV, UKRAINE

RAIS Volodymyr Zelensky wa Ukraine ametaja mashambulio yanayoendelezwa na vikosi vya Urusi katika mji wa Mauripol kuwa “ugaidi” na “uhalifu dhidi ya binadamu.”

Kauli yake ilijiri huku vikosi vya Urusi vikiendelea kudhibiti maeneo mengi katika mji huo muhimu.

“Mbona ufanye hivi kwa mji wenye amani? Ni makosa yapi ambayo wenyeji wamefanya? Huu ni ugaidi ambao utakumbukwa kwa karne nyingi zijazo,” akasema Zelensky kwenye hotuba aliyotoa Jumapili kwa taifa hilo.

Mapigano hayo yamesababisha kituo kimoja cha kutengenezea chuma kufungwa.

Katika mji mkuu, Kyiv, karibu watoto 20 waliobebwa na wanawake waliopewa jukumu la kuwalinda wamekwama katika kambi moja, huku wakingoja wazazi wao halisi kusafiri kutoka maeneo yanayokumbwa na vita ili kuja kuwachukua.

Baadhi ya watoto hao wana umri wa siku kadhaa pekee.

Wengine wanashughulikiwa na wauguzi ambao hawawezi kutoka katika kambi hiyo kutokana na mashambulio yanayoendelea kutekelezwa na Urusi.

Ikiwa vikosi vya Urusi vitaendelea kuudhibiti mji huo na hatimaye kufaulu kuuteka, wadadisi wanasema hiyo itakuwa hatua kubwa kwa Urusi kwenye vita hivyo.

Urusi imekuwa ikijaribu kuiteka miji mikuu nchini humo mara tu baada ya kuanza uvamizi huo Februari 24, 2022, unaotajwa kuwa mkubwa zaidi barani Ulaya tangu kukamilika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia mnamo 1945.

“Watoto na wazee wanafariki. Mji huo umeharibiwa kabisa. Msingi wake umevurugika,” akasema Michail Vershnin, ambaye ni polisi anayehudumu katika mji huo.

Alisema hayo akiwa amejificha kutoka moja ya jengo lililoangushwa na makombora ya Urusi.

Jana Jumapili, Baraza la Mji huo lilisema kuwa vikosi vya Urusi viliishambulia shule moja ya kufunzia sanaa, ambako wenyeji zaidi ya 400 walikuwa wametafuta hifadhi.

Jumamosi, iliibuka kwamba shambulio moja la roketi iliyorushwa na Urusi lilisababisha vifo vya wanajeshi 40 wa maji katika mji wa Mykolaiv, kulingana na afisa mmoja wa kijeshi nchini humo, aliyezungumza na gazeti la The New York Times.

Tayari, vikosi vya Urusi vimefanikiwa kutenganisha mji huo na Ziwa Azov, ambalo huwa muhimu sana kwa shughuli zake za kiuchumi.

Wadadisi wanasema kuanguka kwake kutaliunganisha eneo la Crimea na maeneo yenye wapiganaji waliojitenga na Ukraine.

Hapo jana Jumapili, vikosi vya Ukraine na Urusi vilikabiliana vikali kwenye juhudi za kuchukua udhibiti wa kituo cha kutengeneza chuma cha Mauripol, kulingana na waziri wa Masuala ya Ndani ya Ukraine, Vadym Denysenko.

“Moja ya kituo kikubwa zaidi cha kutengeneza chuma barani Ulaya kinaharibiwa kwa sasa,” akasema Denysenko.

Saa chache baadaye, baraza kuu la mji huo lilisema vikosi vya Urusi viliwahamisha kwa nguvu wanawake na watoto kwa kuwaelekeza nchini mwao.

Mshauri wa Rais Zelensky, Oleksiy Arestovych, alisema kuwa vikosi vya taifa hilo “vinakabiliwa na ugumu mkubwa kuhimili nguvu kubwa ya adui yao (Urusi).”

Licha ya juhudi za Urusi, ripoti zinaeleza kuwa idadi kubwa ya wenyeji bado wako katika jiji hilo.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema inaendelea kuisaidia Ukraine kudhibiti anga yake ili kuhakikisha kuwa hakuna ndege ambayo haijaruhusiwa imepaa.

“Lengo kuu la kwanza la Urusi lilikuwa ni kuchukua udhibiti wa anga ya Ukraine katika siku za mwanzo za uvamizi huo. Hata hivyo, kushindwa kwake kumepunguza makali ya mashambulio yake,” ikasema wizara hiyo kwenye taarifa.