Connect with us

General News

Zoezi kuchagua shule za upili kuanza – Magoha – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Zoezi kuchagua shule za upili kuanza – Magoha – Taifa Leo

Zoezi kuchagua shule za upili kuanza – Magoha

Na WINNIE ATIENO

ZOEZI la kuchagua shule za upili kwa wanafunzi waliopokea matokeo yao ya mtihani wa KCPE, litaanza katika muda wa wiki mbili zijazo, Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema.

Waziri alihakikishia wanafunzi wote waliomaliza masomo ya shule za msingi mwaka huu kwamba watajiunga na shule za sekondari.

Alisema kwamba wote wanaohusika na zoezi hilo wameagizwa kuhakikisha litakuwa huru, haki na lenye uwazi.Prof Magoha alisema hayo akiwa Mombasa jana alipohudhuria kongamano la 24 la Chama cha Madaktari wa Upasuaji Kenya.

Alionya wale ambao watahujumu shughuli hiyo akisema ataisimamia binafsi na kuhakikisha wanafunzi kutoka maeneo ya mbali mashambani wanapata nafasi katika shule za kitaifa.

“Tutahakikisha kwamba watoto wote wa Kenya watachukuliwa sawa na kutendewa haki wakiwemo wale walio mitaa ya mabanda, maeneo kame ya mbali. Tutachukua wale bora kutoka kaunti wajiunge na shule za kitaifa,” alisema waziri.

Hata hivyo, Prof Magoha alisema kwamba watahiniwa wengi wanataka kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za kitaifa ilhali taasisi hizo zinaweza kuwa na nafasi 500 kila moja huku wale waliopata alama zaidi ya 400 katika KCPE wakiwa karibu 12,000.

Lakini waziri alisema kwamba baadhi yao watajilaumu kwa kufanya chaguo lisilofaa kwa kuchagua shule za kitaifa pekee badala ya kuchagua za mkoa na za sekondari kaunti.

“Si lazima uende katika shule kubwa 10 za kitaifa ili uweze kufaulu. Kulingana na matokeo tutakayotoa ndani ya wiki mbili, utaona shule zilizoimarika ni zile ambazo haungefikiria. Kila mtoto yuko salama katika mikono ya Magoha lakini Kenya ni nchi ya ajabu na tunataka kuhakikisha mtoto kutoka Marsabit anapata nafasi Kenya High,” aliongeza Waziri Magoha.

Wakati huo huo, alihakikishia wadau kwamba michezo itarejea muhula huu. Michezo shuleni ilisimamishwa miaka miwili iliyopita kutokana na janga la corona.

Pia alikanusha madai kwamba watahiniwa katika shule za kibinafsi walifanya vyema kuliko wa shule za umma kwa kuwa walidanganya katika mtihani.Matokeo ya KCPE 2021 yalitolewa Jumatatu huku wanafunzi 10 bora wakitoka shule za kibinafsi.

“Mimi ni Waziri wa Elimu sio wa shule za umma au za kibinafsi. Unajua hakukuwa na udanganyifu, matokeo ni kwamba watoto wetu wanafanya vyema. Hakukuwa na wizi katika mitihani ya KCPE na KCSE,” alisema Prof Magoha.

Hata hivyo, waziri alisema kumekuwa na majaribio ya kukiuka uadilifu wa mitihani baada ya karatasi za mitihani kutolewa katika kontena saa kumi na mbili na nusu hata kwa KCSE inayoendelea.

Waziri alisema kwamba wizara yake na idara za usalama zinachunguza suala hilo na kuonya kwamba washukiwa watakabiliwa kisheria.