Connect with us

General News

Zogo kati ya Lenku, Nkedienye kuhusu ugavana lapasua Azimio – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Zogo kati ya Lenku, Nkedienye kuhusu ugavana lapasua Azimio – Taifa Leo

Zogo kati ya Lenku, Nkedienye kuhusu ugavana lapasua Azimio

NA STANLEY NGOTHO

UHASAMA mkali wa kisiasa unatokota kati ya Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku na mtangulizi wake David Nkedienye kuhusu uteuzi pamoja ya kuwania ugavana kupitia vuguvugu la Azimio la Umoja.

Bw Nkedienye amesema hayupo tayari kwa mchujo wa pamoja akisisitiza atawania kiti hicho kupitia ODM. Bw Nkedienye anaungwa mkono na Mbunge wa Kajiado

ya Kati Memusi Kanchori huku wawili hao wakitaka Jubilee pia iwasilishe wawaniaji wake badala ya kuwa na mgombea mmoja kupitia Azimio.

“Mikono yangu hai – jafungwa. Nafuatilia kwa makini matukio yanayoendelea ndani ya Azimio.

“Kile ambacho ni wazi ni kuwa, mimi nitakuwa debeni. Mazungumzo pekee kati yangu na Lenku ni iwapo atashawishika asiwanie ugavana na aendee kiti kingine hasa useneta,” akasema Bw Nkedienye.