[ad_1]
Joao Cancelo wa Man-City avamiwa na wahalifu wanne
Na MASHIRIKA
BEKI Joao Cancelo wa Manchester City alipata mejaraha ya usoni alipokabiliana na wahalifu waliomvamia akiwa na familia yake.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 alipakia kwenye mtandao wa Instagram picha ya kuonyesha jinsi alivyojeruhiwa na wezi hao waliotoweka na vito vya thamani kubwa.
“Yasikitisha kwamba leo niliumizwa na watu wanne waoga walionijeruhi nilipokabiliana nao wakijaribu kudhulumu familia yangu,” akaandika.
“Ukipingana nao, hili ndilo hufanyika. Kwa bahati mbaya, walitoweka na vito vyangu vyote na kuniacha na majeraha haya usoni,” akaendelea.
Cancelo amekuwa sehemu muhimu ya kampeni za Man-City wanaopigiwa upatu wa kuhifadhi ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu.
Alijiumuishwa katika kikosi Bora cha Mwaka cha EPL cha Professional Footballers’ Association (PFA) mnamo 2020-21 baada ya kusajiliwa na Man-City kwa Sh9.3 bilioni kutoka Juventus ya Italia mnamo Agosti 2019.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
[ad_2]
Source link