Connect with us

General News

Wagonjwa wapata taabu mgomo ukianza – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wagonjwa wapata taabu mgomo ukianza – Taifa Leo

Wagonjwa wapata taabu mgomo ukianza

NA SIAGO CECE

HUDUMA za afya katika hospitali za umma na zahanati katika Kaunti ya Kwale zilisitishwa Jumatano, wahudumu wa afya walipoanza mgomo.

Uchunguzi wa Taifa Leo ulibainisha kuwa wagonjwa wengi walilazimika kusubiri kwa saa nyingi kabla ya kutibiwa.

Gavana wa Kaunti ya Kwale, Bw Salim Mvurya, alitishia kuwafuta kazi wale wanaoshiriki mgomo huo.

Akizungumza katika Hospitali ya Kwale, alisema hawana sababu ya kugoma kwa sababu tayari serikali ya kaunti hiyo imeanza kushughulikia matakwa yao.

Kulingana na Gavana, “wahudumu hao watalipwa marupuru na malimbikizo ya mishahara yao ya milioni Sh15.7 wanayodai ifikapo Februari 20”.

Vilevile, alisema kuwa tayari ameidhinisha kupandishwa vyeo kwa wafanyikazi 381 wa afya.

Alisema mchakato wa kubaini idadi ya wahudumu wa afya ambao hawajarejea kazini katika vituo vyote vya afya vilivyoko kaunti hiyo umeanza.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa cha Wauguzi (KNUN) tawi la Kwale, Bw Tobias Onyango, alisema wafanyakazi hao hawatalegea na wataandamana leo Alhamisi asubuhi.

“Hatutaangukia kwenye vitisho. Walitoa ahadi sawia wakati kama huu mwaka jana na wakaishia kutotulipa marupurupu yetu,” alisema Bw Onyango.

Wafanyikazi hao walikuwa wametoa notisi ya mgomo wiki iliyopita.

Wanalalamikia masuala kama vile kuchelewa kupandishwa vyeo na kutolipwa marupurupu kwa miaka mingi.

Wako chini ya vyama tofauti vinavyowakilisha masilahi ya wahudumu tofauti wa afya zikiwemo Muungano wa Kitaifa wa Wauguzi (Knun), Muungano wa Maafisa wa Kliniki (Kuco) Muungano wa Kitaifa wa Maafisa wa Maabara (KNUMLO) na Muungano wa Kitaifa wa Wataalamu wa Teknolojia ya Dawa (KNUPT) miongoni mwa vingine.