Ni makonde ya hadharani sasa kwa Uhuru na Ruto
WANDERI KAMAU NA SHABAN MAKOKHA
NI wazi sasa Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Rais William Ruto wameanza kuelekezeana makombora ya kisiasa moja kwa moja bila kugopana, kinyume na hapo awali ambapo walikuwa wakiwatumia washirika wao.
Mbali na ishara kuwa wawili hao wamekosana kabisa, wadadisi wanasema majibizano hayo yanaonyesha ushindani mkubwa wa kisiasa utakaokuwepo katika uchaguzi wa Agosti 9.
Akihutubu Jumatatu jijini Mombasa alipozindua Mpango wa Afya Kwa Wote, Rais Kenyatta alimkosoa vikali Dkt Ruto kwa kudai amechangia katika mafanikio yaliyofikiwa na seri – kali ya Jubilee, ilhali amekuwa akifanya kampeni tangu 2018.
Rais Kenyatta alimkabili vikali Dkt Ruto, akisema hapaswi kujihusisha kamwe na miradi iliyotekelezwa na serikali yake kwani “alimtoroka kitamb o”.
“Mtindo wa watu kuzungumza maneno matupu huku na huko eti tumefanya hili ama lile umepita. Kazi haifanyiwi juu ya magari. Badala yake, huwa inafanyiwa katika ofisi au hospitalini,” akase ma Rais Kenyatta, akimwelekezea Dkt Ruto, ambaye amekuwa akizuru maeneo mbalimbali nchini akieleza hatua zilizopigwa na serikali katika juhudi za kuboresha maisha ya Wakenya.
Akaongeza, “Wakati wa siasa umefika na mtatusikia. Kila mtu yuko huru sasa. Wale waliotangulia na wale ambao tunaanza. Niliwaambia watu kuwa haya ni kama mashindano ya mbio za marathoni. Hata sisi tumeingia uwanjani.”
Lakini jana, Dkt Ruto alimjibu Rais Kenyatta, akisema hawezi kumtenga kwenye utekelezaji wa miradi ya serikali.
Akihutubu katika eneo Likuyani, Kaunti ya Kakamega, kwenye msururu wa mikutano ya kampeni ya muungano wa Kenya Kwanza Alliance (KKA), Dkt Ruto alisema ametoa mchango mkubwa kwenye mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Jubilee, hivyo hapaswi kutengwa hata kidogo.
“Kama naibu wako, huwezi kunitenga kwenye mafanikio tuliyopata pamoja. Tuliketi chini, tukapanga na tukatekeleza mipango ya ujenzi wa barabara, usambazaji wa umeme, ujenzi wa Taasisi za Kiufundi (TTIs), uimarishaji wa sekta ya elimu na miradi mingine mingi nchini,” akasema Dkt Ruto.
Dkt Ruto alisema Jubilee ni mradi wa pamoja kati yake na Rais Kenyatta, hivyo wanagawana mafanikio na lawama kwa mizani sawa.
“Katika siasa, unapanga kwenye afisi, japo unatekeleza ukiwa nyanjani na wakati mwingine ukiwa juu ya magari,” akaongeza.
Rais Kenyatta anamuunga mkono kiongozi wa ODM, Raila Odinga kuwania urais Agosti chini ya vuguvugu la Azimio la Umoja kumkabili Dkt Ruto, ambaye ameungana na kiongozi wa ANC, Bw Musalia Mudavadi na Seneta Moses Wetang’ula (Ford-Kenya).
Dkt Ruto na washirika wake wamekuwa wakimlaumu Rais Kenyatta kwa “kuwalazimishia” Wakenya kumchagua Bw Odinga, wanayemtaja kama “mradi” wa serikali.
Next article
Sheria za kuandaa ‘Mutura’ kubuniwa Murang’a