Connect with us

General News

Afueni wanafunzi wa msitu wa Boni wakirejea shuleni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Afueni wanafunzi wa msitu wa Boni wakirejea shuleni – Taifa Leo

Afueni wanafunzi wa msitu wa Boni wakirejea shuleni

NA KALUME KAZUNGU

KWA UFUPI

  • – Walikuwa wamesalia nyumbani kwa zaidi ya mwezi mmoja.
  • – Walikuwa wa vijiji vya Basuba, Milimani, Mararani, Mangai na Kiangwe.
  • – Takriban wanafunzi 200 husafirishwa kutoka vijijini kwao hadi shule ya bweni ya Mokowe Arid Zone ili kuendeleza masomo yao.
  • – Wanafunzi hao walisafirishwa kwa boti iliyofadhiliwa na Serikali ya Kaunti ya Lamu.

WANAFUNZI zaidi ya 100 kutoka vijiji vya msitu wa Boni ambao walikuwa wamesalia nyumbani licha ya shule kufunguliwa kwa masomo ya muhula wa tatu, zaidi ya mwezi mmoja uliopita, hatimaye wamerudi madarasani.

Wanafunzi hao wa kati ya gredi ya 3 na darasa la nane kutoka vijiji vya Basuba, Milimani, Mararani, Mangai na Kiangwe hawakuwa wamerudi shuleni kuendeleza masomo yao kama wengine nchini kutokana na tatizo la kiusalama na usafiri.

Takriban wanafunzi 200 kutoka vijiji vya msitu wa Boni, hasa wale wa madarasa ya juu, kila muhula

unapoanza hulazimika kusafirish – wa kutoka vijijini kwao hadi shule ya msingi ya bweni ya Mokowe Arid Zone ili kuendeleza masomo yao kwenye mazingira salama.

Aidha, tangu muhula wa tatu kufuanza Januari 4 mwaka huu, ni wanafunzi 100 pekee kutoka msitu wa Boni ambao walikuwa wamefika shuleni hali 100 wengine walikuwa wamesalia majumbani kutokana na ukosefu tatizo la usafiri na pia utovu wa usalama ulioshuhudiwa Lamu karibu wiki tatu zilizopita.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Mokowe Arid Zone, Bw Charles Mzee, jana alithibitisha kupokea wanafunzi wote kutoka vijiji vya msitu wa Boni shuleni humo mwishoni mwa juma lililopita.

Wanafunzi hao walisafirishwa kwa boti iliyofadhiliwa na Serikali ya Kaunti ya Lamu hadi katika shule hiyo ya bweni.

“Ninashukuru kwamba wanafunzi wangu wote waliokuwa wamesalia kwenye vijiji vya msitu wa Boni kwa sasa wako shuleni. Hata tumepata wanafunzi wengine wageni kutoka vijiji vya msitu wa Boni.

Masomo kwa sasa yanaendelea vyema shuleni,” akasema Bw Mzee.

Afisa Mkuu wa Kitengo cha kush – ughulikia Majanga kwa Serikali ya Kaunti ya Lamu, Bw Shee Kupi, aliyeongoza shughuli ya kuwasafirisha wanafunzi hao kutoka msitu wa Boni alisema haikuwa rahisi kwao kuwafikia wanafunzi hao vijijini na kuwarudisha shuleni.