Connect with us

General News

Wazee wagawanyika kuhusu ugavana Tana River – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wazee wagawanyika kuhusu ugavana Tana River – Taifa Leo

Wazee wagawanyika kuhusu ugavana Tana River

NA STEPHEN ODUOR

TOFAUTI zimeibuka katika baraza la wazee wa jamii ya Waorma, Kaunti ya Tana River kuhusu kiongozi anayestahili kutawazwa kuwania ugavana.

Mbunge wa Bura, Bw Ali Wario, aliteuliwa kuwania ugavana na baadhi ya wazee wa jamii hiyo Ijumaa, katika kijiji cha Dibe.

Jopo hilo la wazee wanane likiongozwa na mwenyekiti Omar Gobe, lilimteua Bw Wario katika hafla ndogo eneobunge la Tana Delta, na kumbariki kupeperusha bendera ya jamii hiyo.

Hata hivyo wazee wengine wa baraza hilo la wazee walipinga uamuzi huo, hali iliyozua sintofahamu.

Walalamishi waliandaa mkutano maalum katika makao makuu ya jamii ya Orma katika kijiji cha Wayu Boru ambapo walifanya maamuzi mapya na kumteua Waziri Msaidizi wa Usalama

Hussein Dado kuwa mwaniaji wa ugavana atakayeungwa na jamii.

Akizungumza baada ya shughuli hiyo, Mzee Dibe Barisa aliwakashifu wazee waliomtawaza Ali Wario akisema kuwa wanane hao waliinajisi katiba ya jamii kwa kwenda kinyuma na fungu zake.