[ad_1]
Amri mzee, 76, asiuze nyumba ya jamaa yake
Na JOSEPH WANGUI
MAHAKAMA kuu imetupilia mbali ombi la mwanamume mwenye umri wa miaka 76, aliyekuwa anataka kuuza boma la familia lenye thamani ya Sh70 milioni bila idhini kutoka kwa mke wake.
Mzee huyo aliwasilisha kesi mahakamani mnamo 2017 akitaka kufutiliwa mbali kwa Kipengele 7 na 12 cha Sheria kuhusu Umilisi wa Mali ya ndoa (2013) baada ya mkewe kupinga hatua ya kuuza boma lao katika eneo la Loresho, Nairobi.
Mwanamume huyo kwa lakabu ya M.K.G. alikusudia kumpa mke wake asilimia 20 ya fedha atakazopata kutokana na mauzo hayo.Alikuwa ameihimiza korti kupiga marufuku vipengele hivyo viwili vya sheria kama vinavyokiuka katiba.
Hata hivyo, Jaji Agrey Muchelule alirusha nje kesi hiyo jana kwa misingi kuwa madai ya ukiukaji wa haki unahusu watu wawili na kwamba Mwanasheria Mkuu hakuhusika katika vikao vya kusikilizwa kwa kesi hiyo.Korti ilimweleza mwanamume huyo kuwa mkewe huenda asiweze kutetea ufaafu kikatiba wa vipengele hivyo vya sheria vinavyopingwa.
“Ni Mwanasheria Mkuu pekee anayeweza kutetea maslahi ya umma katika vipengele hivyo na kutetea maslahi ya Bunge la Kitaifa lililopitisha Sheria na vipengele hivyo. Ni lazima mtu akumbuke dhana kwamba sheria zote zinazopitishwa na Bunge ni za kikatiba mradi haijathibitishwa vinginevyo,” alimuru Jaji Muchelule.
Mahakama ilielezwa kuwa mwanamume na mwanamke huyo kwa lakabu ya E.G, wangali wanaishi pamoja kama mume na mke na wameoana. Walifunga ndoa Julai 8, 1978 na wana watoto watatu.Wanandoa hao wana mali kadhaa ikiwemo boma la ekari nne kijijini Nyeri, jumba la kibiashara eneo la Giakanja na jumba la kupangisha Kajiado.
Mzee huyo alieleza korti kuwa amestaafu na hana raslimali nyingi akisema kuwa alinunua boma lao la Loresho akitumia pesa alizochangia mkewe.
Next article
TAHARIRI: Njaa haifai kusumbua miaka 58 tangu uhuru
[ad_2]
Source link