[ad_1]
Ashtakiwa kumlaghai yaya Sh0.2M
Na RICHARD MUNGUTI
MFANYABIASHARA ameshtakiwa kwa kumlaghai Yaya anayefanya kazi nchini Saudi Arabia Sh232,770 akidai atamsaidia kuanzisha biashara.
Wesley Imbunya alishtakiwa mbele ya hakimu mkazi William Tullel kwa kupokea pesa kwa njia ya udanganyifu. Alikana alimtapeli Maureen Khavungwi pesa hizo kati ya Aprili 2020 na Desemba 2021 mtaani Kangemi Nairobi Biashara aliyoahidiwa Khavungwi iligeuka kuwa upepo ndipo akafahamisha polisi.
Uchunguzi ulibaini mshtakiwa alitumia pesa hizo alizotumiwa na Khavungwi aliyekuwa anafanyakazi nchini Saudi Arabia kama Mjakazi. Mlalamishi alikuwa anatuma pesa hizo kutoka akaunti yake Saudi Arabia hadi kwa akaunti ya mshtakiwa nchini Kenya katika benki ya Kingdom Bank iloyoko Nairobi.
Imbunya aliachiliwa kwa dhamana ya Sh300,000. Pia alielezwa anaweza kulipa dhamana ya pesa tasilimu Sh50,000 hadi Feburuari 22,2022 itakapotajwa.
[ad_2]
Source link