Khalwale aliwashambulia viongozi wa Magharabi ya Kenya kwa kumtembelea Uhuru na kutoka huko na basi. Picha: Boni Khalwale. Source: Facebook
Awali TUKO.co.ke iliripoti kuwa kiongozi wa taifa alikutana na viongozi hao jumba la Harambee Nairobi Jumatano, Julai 1 ambapo alimpa Mwenyekiti wa kampuni ya sukari ya Nzoia Sugar Joash Wamang’oli basi.
Viongozi waliohudhuria mkutano huo walikuwa magavana Wycliffe Oparanya (Kakamega), Sospeter Ojaamong (Busia), Wycliffe Wangamati (Bungoma), Wilber Ottichilo (Vihiga) na Patrick Khaemba (Trans-Nzoia).
Wengine ni Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa na Katibu wa COTU Francis Atwoli.
Kulingana na Khalwale, viongozi walipaswa kuitisha mambo ya maendeleo kama ongezeko la mgao wa bajeti kwa kaunti za Busia, Kakamega, Bungoma, Trans Nzoia na Vihiga ambazo kwa jumla zilitengwa KSh bilioni 40 katika mwaka wa Fedha wa 2019/2020.
“Licha ya kaunti za Busia, Kakamega, Bungoma Vihiga na Trans Nzoia kupokea bajeti ya KSh bilioni 40 kwa pamoja mwaka wa fedha wa 2019/20, jana, viongozi wetu walikwenda kwa Rais kuomba basi! Ni masikitiko makubwa. Wana bahati Uhuru hakuwachezea kama Sonko,” mwanasiasa huyo alidokeza.
Matamshi yake yalimkwaruza Atwoli ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akileta umoja katika eneo la Magharibi ya Kenya kabla ya kura ya maoni katika mchakato wa Building Bridges Initiative.
Atwoli alipuzilia mbali matamshi ya Khalwale na kusema akili yake sio timamu. Picha: Franciz Atwoli. Source: Facebook
“Mtu yeyote anayeweza kudhani kwamba viongozi tajika pamoja na kiomgozi wa nchi wanaweza kukutana juu ya basi hakika anahitaji kuonana na daktari. Huyo akili zake sio timamu,” akajibu Atwoli.
Majibizano hayo yalizua mdahalo mkali miongoni mwa wafuasi wao huku baadhi wakikubaliana na mwanasiasa huyo na wengine wakimuunga mkono katibu huyo.