Judith Nyambura Mwangi almaarufu Avril ni mama wa mtoto mmoja ambaye alijifungua mwaka jana. Si mama tu wala ni msanii wa nyimbo, mwandishi wa nyimbo pia na ni muigizaji wa vipindi tofauti.
Avril akiwa katika mahojiano na Massawe Japanni alisema kuwa kulikuwa na uvumi kuwa J Blessings ndiye alikuwa baba wa mtoto wake na kwamba kuwa ni uvumi.
“Baba yangu alipinga sana kazi yangu ya kuwa msanii kwa maana nilikuwa na shahada ya (Product and design),
“Niliweza kuhitimu katika chuo kikuu cha Nairobi, nilianza kupenda kuwa msanii nikiwa katika shule ya upili,” Alisema Avril.
Avril alisema kuwa aliweza kusikia vyema alipokuwa mama kwa maana ni jambo ambalo alikuwa amelingoja kwa muda mrefu.
Msanii huyo aliweza kusema pia baada ya miezi mitatu baada ya kuzaa aliweza kurudi katika kazi yake, alisema kuwa mama ina changamoto ambazo anajaribu kupambana nazo.
Pia Avril aliweza kukanusha madai kuwa alizaa kupitia oparesheni bali alizaa kwa njia mwafakakwa hivyo ni uvumi tu pekee.
“Nilizaa kawaida sikufanyiwa oparesheni kwa hivyo kwa wale wanasema nilifanyiwa oparesheni si ukweli,” Avril aliongea.
Aliweza kusema kuwa baba wa mtoto wake uwa anamsaidia pia huwa anaenda kumuona mtoto huyo na kwa sasa wako katika suala nzuri na baba wa mtoto.