Connect with us

General News

Blak Blad yaosha Homeboyz raga ya Kenya Cup – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Blak Blad yaosha Homeboyz raga ya Kenya Cup – Taifa Leo

Blak Blad yaosha Homeboyz raga ya Kenya Cup

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya Blak Blad ya Chuo Kikuu cha Kenyatta imemaliza mikosi ya kutoshinda mchuano kwenye Ligi Kuu ya raga ya wachezaji 15 kila upande (Kenya Cup) simu 2021-2022 baada ya kulipua Homeboyz kwa pointi 28-0 ugani KCB Ruaraka jijini Nairobi, Jumamosi.

Vijana wa kocha Motto Williams, ambao hawakuwa pia wamepiga ‘madeejay’ hao tangu waandikishe ushindi wa 13-12 katika ligi ya daraja ya pili mwaka 2010, walivuna ushindi huo muhimu kupitia mchezaji wa timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande ya Shujaa, Archadius Khwesa aliyetinga miguso mitatu.

Derrick Wechuli pia alichangia miguso miwili naye nahodha Lionel Ekesa akapachika penalti. Blak Blad, ambayo ilianza msimu kwa kukung’utwa 49-3 Novemba 27, sasa ina alama tano.

Imeongeza masaibu ya Homeboyz ambayo ilichabangwa 18-10 na mabingwa watetezi KCB katika mechi ya ufunguzi mnamo Novemba 27 na kupoteza 22-17 dhidi ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknoloji cha Masinde Muliro (MMUST) mnamo Desemba 4.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending