Naibu Rais William Ruto anaendelea kujipanga kwa siasa za 2022. Picha: William Ruto Source: Facebook
Kulingana na gazeti la Nation, DP tayari amempata aliyekuwa mkuu wa wafanyakazi katika afisi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga wakali wa serikali ya mseto Caroli Omondi.
Omondi inaarifiwa ni mmoja wa wanakamati 16 ambao wamejiunga chini ya mwavuli wa ‘kamati ya vita’ vya DP kwenye safari ya urais 2022.
Kamati hiyo ni ya watu waliotajika kwenye nyanja mbali mbali na kazi yao kwa sasa ni kuhakikisha Ruto anatwaa urais 2022.
Aliyekuwa mkuu wa wafanyakazi katika afisi ya Raila Odinga wakati wa serikali ya Mseto Caroli Omondi. Omondi kwa sasa ameingia kambi ya DP Ruto. Picha: Caroli Omondi Source: Facebook
Wengine kenye kamati hiyo ni wanasiasa Bonny Khalwale, Johnson Muthama na aliyekuwa seneta wa Mombasa Hassan Omar.
Khalwale alisema kutakuwa na wimbi kali mara tu janga la covid-19 litatulia na mahasimu wa DP Ruto watashtuka.
“Tutawashangaza mahasimu wetu wakati tu kafyu ya kutosafiri itaondolewa,” alisema Khalwale.
Aliyekuwa Seneta wa Machakos Johnson Muthama sasa ni mmoja wa kamati inayounda mikakati ya DP Ruto kuingia Ikulu 2022. Picha: Citizen Source: UGC
“Kuna mirengo miwili pekee Kenya ambao itashindana kwenye mbio za urais, mmoja ukiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga na kiongozi wa Kanu Gideon Moi na mwingine wa Ruto na Wakenya,” alisema Muthama
David Mugonyi, Emmanuel Tallam na Dennis Itumbi inaarfiwa watakuwa wanashughulikia mawasiliano ya DP kwenye kamati hiyo.
Wengine ni aliyekuwa waziri Davis Chirchir, Korir Sing’oei ambaye atashughulikia masuala ya kisheria na Augustine Cheruiyot ambaye atamshauri DP kuhusu uzalishaji wa chakula humu nchini.