Connect with us

General News

Jinsi ya kuandaa katlesi za kuku – Taifa Leo

Published

on


Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa Mapishi: Dakika 20

Walaji: 4

Vinavyohitajika

 • nyama ya kuku nusu kilo; iwe bila ngozi na mifupa
 • juisi ya ndimu 1
 • chumvi
 • pilipili manga kiasi
 • mafuta ya kupikia vijiko 3
 • viazi 5
 • kitunguu maji kilichokatwakatwa
 • kitunguu saumu kilichotwangwa kijiko 1
 • tangawizi iliyotwangwa kijiko ½ cha chai
 • binzari ya unga kijiko 1
 • Garam masala kijiko ½ cha chai
 • pilipili mbichi iliyokatwa vipande vidogovidogo
 • manjano kijiko ½ cha chai
 • giligilani ya unga kijiko ½
 • majani ya kotmiri yaliyokatwakatwa vijiko 2
 • mayai 2, piga tia katika bakuli
 • chenga za mkate kiasi; ziwe kwenye sahani

Maelekezo

Tia kuku pamoja na mahitaji yake yote katika sufuria iliyoinjikwa mekoni na uchemshe kama kawaida hadi nyama hiyo iive vizuri.

Chemsha viazi ukiwa umeweka chumvi kiasi kwenye maji utakayotumia kisha chuja maji yote na uviponde viazi hivyo.

Mnyambue kuku kupata vipande vidogovidogo. Unaweza pia kuisaga minofu kwenye blenda ya vitu vikavu.

Tia mafuta kwenye sufuria juu ya meko yenye moto wa kiasi. Yakipata moto weka vitunguu na kaanga hadi vianze kupata rangi.

Tia tangawizi na kitunguu saumu pamoja na maji kidogo kisha kaanga hadi vitoe harufu.

Tia manjano na chumvi kiasi halafu koroga vizuri kisha tia kuku na kaanga tena kwa dakika mbili. Sasa tia viazi vyako ulivyoponda na uchanganye vizuri.

Tia viungo vilivyobaki kisha koroga vizuri. Onja chumvi ujue kama ipo sawa au uongeze kama itahitajika.

Weka majani ya kotmiri. Funika kisha pika kwa dakika moja. Epua na acha mchanganyiko upoe.

Chota mchanganyiko wako ufanye madonge kisha taratibu finya kwa kiganja chako kufanya umbo. Panga katika sahani.(Unaweza fanya shepu yoyote).

Mimina mafuta katika sufuria iliyo mekoni. Hakikisha moto ni wa kiasi. Mafuta yakipata moto, chovya katlesi katika mayai kisha zungusha katika chenga za mkate na tia katika mafuta moto.

Kaanga hadi zipate rangi nzuri ya hudhurungi pande zote mbili. Epua katika chujio zichuje mafuta.

Pakua na ufurahie.Source link

Comments

comments

Facebook

Trending