Connect with us

General News

Jinsi ya kuandaa masala ya nyama ya ng’ombe – Taifa Leo

Published

on


MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa masala ya nyama ya ng’ombe

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 0

Walaji: 3

Vinavyohitajika

 • nyama ya ng’ombe kilo 1
 • nyanya 3 zilizosagwa
 • kitunguu maji
 • kitunguu saumu, tafuta punje 5 za aina hii ya vitunguu
 • tangawizi kijiko 1
 • unga wa pilipili nyekundu
 • mtindi kikombe ½
 • hiliki
 • mdalasini
 • mafuta ya kupikia
 • chumvi kiasi unachopenda
Nyama ya ng’ombe kabla ya kukatwa vipande vidogovidogo. PICHA | MARGARET MAINA

Maelekezo

Menya tangawizi na vitunguu saumu kisha vitwange.

Katakata nyama yako vizuri kisha ioshe.

Weka nyama kwenye bakuli kubwa au sufuria kisha mimina mafuta ya kupikia. Kisha weka tangawizi, kitunguu saumu, pilipili manga, unga wa pilipili nyekundu (red pepper), mtindi, hiliki, na mdalasini. Baada ya hapo, changanya na uache mchanganyiko huo kwa muda wa saa nne ili nyama ilainike.

Muda huo ukishaisha, washa moto na uweke sufuria mekoni. (Hakikisha moto ni mkali kiasi)

Weka mafuta kiasi kwenye sufuria.

Weka kitunguu maji kisha koroga hadi kiwe kahawia.

Weka mchanganyiko wa nyama na viungo vingine.

Funika.

Acha nyama ichemke kwa dakika 15 kisha koroga.

Funika na usubiri kwa muda wa dakika 10 hivi.

Punguza moto kidogo na acha kwa dakika 15 nyingine.

Angalia kama nyama imelainika. Ikiwa iko tayari, basi ni wakati mwafaka wa kuiepua.

Pakua na ufurahie kwa ama wali, chapati, ugali au chochote ukipendacho.Source link

Comments

comments

Facebook

Trending