[ad_1]
Jinsi ya kuandaa mishikaki ya maini
Na MARGARET MAINA
[email protected]
Muda wa kuandaa: Dakika 10
Muda wa mapishi: Dakika 20
Walaji: 4
Vinavyohitajika
maini kilo 1
tangawizi vijiko 2
pilipili kiasi
kitunguu saumu kijiko 1
chumvi kiasi
ndimu vijiko 2 vya chakula
beef masala kijiko cha chakula
karoti 1
mafuta kikombe ¼
Maelekezo
Osha maini vizuri.
Kata maini kwa urefu kisha kata vipande vikubwa kiasi
Jitahidi usikate vipande vidogo kwa sababu mishikaki ukiichoma ina kawaida ya kusinyaa (inakuwa midogo baada ya kuiva).
Weka viungo vilivyotajwa hapo juu isipokuwa mafuta na karoti.
Weka kwenye jokovu kwa muda wa saa moja au zaidi ili ipate kulainika. Ukiitoa ichanganye vizuri.
Katakata karoti kwa umbo la duara.
Chukua vijiti vya mishikaki, weka maini matatu yaachanishwe na karoti.
Weka jikoni kwa ajili ya kuioka kwa kutumia ovena ila unaweza kutumia jiko lolote.
Panga kwenye kifaa cha kuchomea kisha tumia brashi kupaka mafuta mishikaki yako.
Weka moto wa nyuzijoto 150 kwa kipimo cha sentigredi, moto wa juu na chini. Oka kwa dakika 20.
Kisha igeuze huku ukipaka mafuta tena oka kwa dakika 15 tu.
Hakikisha hauipiki kwa muda mrefu hadi ikakauka na kukakamaa.
Pakua na ufurahie na chochote kama slesi za mkate, wali na kadhalika.
[ad_2]
Source link