MALENGE ni zao ambalo ni muhimu kiafya kutokana na sifa zake kuwa na vitamini kwa wingi na nyuzinyuzi.
Je, unajua kwamba unaweza kutumia malenge kutengeneza supu na hata krimu unayoweza kupaka kwa slesi za mkate?
Muda wa kuandaa: Dakika 10
Muda wa mapishi: Dakika 15
Walaji: 3
Vinavyohitajika
Malenge kilo 1
Maji vikombe 4
Kitunguu
Kitunguu saumu punje 5 ambazo unatakiwa uwe umeziponda
Vijiko 2 vya tangawizi kavu
Krimu ya kupikia gramu 250
Nyanya 2
Pilipili
Majani ya giligilani
Maelekezo
Osha malenge na uanze kuchonga kisha ukate vipande vidogovidogo.
Weka mafuta ya kupikia kwenye sufuria mekoni na yakishapata moto, weka vitunguu vilivyokatwa na uache viive vizuri kwa muda wa dakika tano mpaka vilainike lakini visiwe na rangi.
Ongeza kilo moja ya hivyo vipande vya malenge kwenye sufuria, kisha endelea kupika kwa dakika 10 huku ukikoroga mara kwa mara. Mchanganyiko huo utalainika na kugeuka rangi ya kahawia.
Mimina mililita 700 za mchuzi wa kuku kwenye sufuria na uweke chumvi na pilipili kiasi. Koroga na uendelee kupika kwa dakika 15.
Mimina mililita 150 za krimu ya kupikia kwenye sufuria, urejeshe kuchemsha, kisha suuza kwenye blenda kwa dakika mbili.
Pakua na ufurahie supu ya malenge.
Unaweza kuila kwa mkate.
Supu ya malenge na slesi za mkate. PICHA | MARGARET MAINA