Naibu Rais William Ruto katika mkutano wa awali na vijana nyumbani kwake Karen. Picha: William Ruto Source: Facebook
“Nimekuwa na chakula cha mchana na wabunge wa Jubilee ambao hivi karibuni walitolewa kwenye nyadhifa zao na kupewa wajibu mwingine. Niliwashukuru kwa kazi yao kwa chama na taifa,” alisema DP kuhusu mkutano wake na wabunge hao katika makao ya Jubilee Asili.
Huku kauli mbiu ya chama cha Jubilee ikiwa ni ‘Tuko Pamoja’, DP alimalizia ujumbe wake ‘Sote Pamoja’ katika kile kiliashiria usemi wa chama hicho kipya.
Seneta Kipchumba Murkomen alisema hakuna nia ya kuunda chama mbadala na Jubilee. Picha: Kipchumba Murkomen Source: Facebook
Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen, hata hivyo, alisema Jubilee Asili si chama kingine mbali ni nyumba ya wanaoamini kuhusu ajenda ya awali ya Jubilee.
“Tulikuwa na mkutano na DP katika jumba la Jubilee Asili Centre. Ni makao ya wanachama wote si chama mbadala kwa Jubilee.
Ni makao ya wanachama wanaoamini kuhusu ajenda ya awali ya Jubilee,” Murkomen alisema.
Caleb Kositany alisema watasajili Jubilee Asili kama chama chao cha kisiasa. Picha: Standard Source: Facebook
Hata hivyo, Mbunge wa Soy Caleb Kositany ambaye pia ni naibu katibu wa Jubilee alisema kuna mipango ya kusajili Jubilee Asili kama chama cha kisiasa.
“Sisi kwa Jubilee hakuna demokrasia, hakuna tena kujadiliana, imekuwa ni kama klabu ya watu wachache ambapo wanachama wanaamriwa kile watafanya. Kama hawatapinga kusajiliwa, basi tutakuwa na chama cha Jubilee Asili,” alisema Kositany.