Connect with us

General News

Kinoti lazima aende jela, asisitiza jaji – Taifa Leo

Published

on


Kinoti lazima aende jela, asisitiza jaji

Na RICHARD MUNGUTI

JUHUDI za Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) George Kinoti za kukwepa jela ziliambulia patupu Jumatatu Mahakama Kuu ilipokataa kufutilia mbali agizo la kumtaka atumikie kifungo cha miezi minne gerezani.

Hili lilikuwa jaribio la nne kwa Bw Kinoti kuomba korti ifutilie mbali uamuzi huo.

“Uamuzi wa mahakama wa Novemba 11 kwamba, Kinoti atumikie kifungo cha miezi minne utasalia. Anatakiwa kujisalamisha kwa idara ya magereza kama alivyoagizwa,” Jaji Antony Mrima alisema Jumatatu.

Jaji Mrima alitupilia mbali ombi la Bw Kinoti kupitia kwa wakili Cecil Miller kwamba, ni “bodi ya silaha ambayo inafaa kushtakiwa kwa vile silaha zinazotolewa kwa umma wanaopewa leseni hazihifadhiwi katika afisi yake.”

Bw Miller alisema bodi inayohusika na uhifadhi wa silaha ndiyo ingeshtakiwa na wala sio mkurugenzi huyu.Source link

Comments

comments

Facebook

Trending