Connect with us

General News

KNEC yapuuzilia uvumi kwamba KCSE na KCPE imeahirishwa – Taifa Leo

Published

on


KNEC yapuuzilia uvumi kwamba KCSE na KCPE imeahirishwa

Na CHARLES WASONGA

BARAZA la Kitaifa la Mitihani (KNEC) limepinga madai yanayosambazwa mitandaoni kwamba limeahirisha tarehe ya kufanyika kwa mitihani ya kitaifa iliyoratibiwa kufanyika Machi 2022.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Jumatano, baraza hilo limeshikilia kuwa Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) na ule wa Daraza la Nane (KCPE) haijaahirisha na itafanyika kuanzia Machi hadi Aprili. “Tungependa kuwajulisha wadau wote kwamba hakuna mabadiliko yoyote katika tarehe za mitihani ya KCPE na KCSE,” akasema Afisa Mkuu Mtendaji wa KNEC David Njegere.

Uvumi huo ulichipuza kufuatia pendekezo la walimu wakuu wa shule za upili kwamba mitihani iahirishwe kwa miezi miwili ili kutuliza msururu wa visa vya utovu wa nidhamu shuleni. Mali ya thamani kubwa ya shule hizo za mabweni imeharibiwa katika visa vya wanafunzi kuteketeza majengo ya shule, haswa wa mabweni.

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wakuu wa Shule za Upili (KESSHA) Kahi Indimuli alinukuliwa akisema kuwa wanafunzi wa kidato cha nne huenda hawako tayari kufanya mtihani wa KCSE na ndio maana wanateketeza shule.

“Watahiniwa wa sasa walikuwa katika kidato cha tatu mwaka jana, na huenda kukaa kwao nyumbani kwa muda mrefu wenzao wa kidato cha nne waliporejelea masomo Oktoba 5, 2020 kuliwaathiri kwa njia nyingi. Kwa hivyo, wanafunzi hawa sasa wameingiwa na woga wa mtihani na ndio maana wameamua kuzuia fujo,” akaeleza Bw Indimuli ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Upili ya Wavulana ya Machakos.

Ni baada ya kutolewa kwa pendekezo hilo la Kessha ambapo watu fulani walianza kusambaza uvumi kupitia mitandao ya kijamii kwamba KNEC imeahirisha mitihani ya kitaifa. Kwa upande wake ,Waziri wa Elimu George Magoha amewataka wanafunzi kuwa watulivu akisema mitahani tayari imetayarishwa na “haitakuwa ngumu zaidi.”

Mwaka jana, KNEC iliahirishwa mitihani ya kitaifa kutokana na mlipuko wa janga la Covid-19 ambalo lilichangia shule zote kufungwa kwa muda usiojulikana.Source link

Comments

comments

Facebook

Trending