Connect with us

General News

Kongole watimkaji marathon kutuletea sifa tena – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kongole watimkaji marathon kutuletea sifa tena – Taifa Leo

TAHARIRI: Kongole watimkaji marathon kutuletea sifa tena

Na MHARIRI

WIKI iliyopita wakimbiaji Philemon Kiplimo, Collins Koros na Sheila Chepkirui waliwika katika Bahrain Night Half Marathon na kufanya taifa letu kuendelea kutambulika kote duniani tena.

Kiplimo alijizolea Sh3.3 milioni baada ya kuponyoka na taji la mbio za Bahrain Royal Night Half Marathon nchini Bahrain Jumapili iliyopita usiku.

Alifuatwa na Kibiwott aliyeweka rekodi ya dunia 57:32 kwenye Valencia Half Marathon 2020. Katika kitengo cha kina dada, Sheila Kiprotich alitawala.

Siku moja kabla, Mark Korir alikuwa ametwaa ubingwa wa mbio za Zurich Malaga Marathon mjini Malaga nchini Uhispania huku Beatrice Cheptoo akichukua nafasi ya tatu katika kitengo cha kina dada.

Mnamo Desemba 5 Nancy Jelegat alishinda mbio za kilomita 42 katika Valencia Marathon nchini Uhispania upande wa kinadada huku Lawrence Cherono akibeba taji upande wa wanaume.

Mbali na hawa waliotamba majuzi, hali ya kukwagura mataji ya mbio ndefu ilishuhudiwa mara chungu nzima mwaka huu.

Benson Kipruto na Diana Kipyokei walitawala mbio za Boston Marathon nchini Amerika mnamo Oktoba 11.

Mshikilizi wa rekodi ya zamani ya Nusu-Marathon duniani Joyciline Jepkosgei alinyakua taji la London Marathon nchini Uingereza mnamo Oktoba 3.

Bethwel Yegon alikamata nafasi ya pili Berlin Marathon nchini Ujerumani mnamo Septemba 26.

Bingwa wa dunia Ruth Chepng’etich alipata umalkia wa Chicago Marathon nchini Amerika mnamo Oktoba 10.

Albert Korir na Peres Jepchirchir waliponyoka na mataji ya New York Marathon mnamo Novemba 7.

Peres Jepchirchir na Eliud Kipchoge pia walishinda marathon kwenye Olimpiki mnamo Agosti 8 mjini Sapporo, Japan.

Tunapoendelea kufunga mwaka wa 2021, ni vyema kuwapongeza washindi na pia waliopoteza kishujaa baada ya kujitolea kuwakilisha nchi kwa ukakamavu.

La muhimu ni kukumbatia sifa hizo huku zikitupa motisha kupanua na kupalilia vipawa vyetu ili kufikia ufanisi mkubwa zaidi mwaka 2022.

Si siri kwamba siku hizi mbio na michezo kwa jumla ni mojawapo ya nafasi za ajira ambazo zinalipa vyema na vijana hawana budi kuiga mara moja.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending