[ad_1]
Maskwota Lamu watishia kususia uchaguzi mkuu
NA KALUME KAZUNGU
MASKWOTA katika Kaunti ya Lamu wametisha kususia uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022 wakidai wamekosa imani na viongozi wao.
Maskwota hao wanadai wanasiasa wa Lamu huwajia kuomba kura kila wakati uchaguzi mkuu unapowadia na punde wanapoingia uongozi huwasahau.
Msemaji wao, Bw Kombo Abushir, alisema kwa miaka mingi wanaendelea kuhangaika wakitafuta makao ilhali viongozi wao huwahadaa bila usaidizi.
Serikali ya kaunti ya Lamu, kupitia kwa gavana Fahim Twaha, mnamo 2017 ilikuwa imeahidi kuhakikisha angalau maskwota 20,000 wa Lamu wapate hatimiliki kufikia mwishoni mwa kipindi cha awamu yake ya kwanza.
[ad_2]
Source link