[ad_1]
Mbunge wa Ugenya ahamia kambi ya Seneta Orengo
NA KASSIM ADINASI
SENETA wa Siaya James Orengo amepata nguvu mpya baada ya azma yake ya kutaka kuwa gavana kuungwa mkono na kiongozi wa chama cha MDG David Ochieng.
Bw Ochieng ambaye ni mbunge pekee aliyechaguliwa kupitia chama tofauti na ODM katika Kaunti ya Siaya, alikuwa akiunga mkono mbunge wa zamani wa Rarieda Nicholas Gumbo anayewania ugavana kupitia chama cha United Democratic Movement (UDM).
Hatua hiyo ya Bw Ochieng inamaanisha kuwa Bw Orengo sasa anaungwa mkono na wabunge wote katika Kaunti ya Siaya.
“Tulikuwa tunaunga mkono Bw Gumbo lakini alitusaliti kwa kujiunga na chama kidogo cha UDM. Tumeachana naye na sasa tumehamia kwa Bw Orengo,” akasema Bw Ochieng.
Alisema kuwa chama chake cha MDG hakitasimamisha mwaniaji wa ugavana katika Kaunti ya Siaya.
“Lakini viti vingine tutasimamisha wawaniaji wa viti vilivyosalia,” akasema.
Alikejeli UDM akisema kuwa ndicho chama kidogo zaidi ndani ya muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya.
Aliyekuwa msemaji wa polisi Charles Owino aligura ODM na kujiunga na UDM na kutangaza kuwa mwaniaji mwenza wa Bw Gumbo.
[ad_2]
Source link