Mwakilishi Wadi kutoka Kaunti ya Kitui, James Munuve aliandikisha ripoti polisi baada ya kupigwa hadharani kwa kushinikiza kung’olewa mamlakani kwa Gavana Charity Ngilu.
Munuve, ambaye anawakilisha wadi ya Kanziku, alisimulia kuwa alivamia na jamaa mmoja akiwa hotelini.