Connect with us

General News

Mlalamishi aondoa kesi ya kupinga azma ya Sonko – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mlalamishi aondoa kesi ya kupinga azma ya Sonko – Taifa Leo

Mlalamishi aondoa kesi ya kupinga azma ya Sonko

NA PHILIP MUYANGA

MMOJA wa walalamishi wawili waliotaka aliyekuwa gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko, azuiwe kuwania ugavana Mombasa, amewasilisha ombi kujiondoa kwa kesi hiyo.

Bw Ndoro Kayuga, aliambia Mahakama ya Mombasa kwamba ametambua Bw Sonko aling’olewa mamlakani kisiasa kwa hivyo huenda kesi iliyowasilishwa ni dhaifu kisheria.

Alidai kuwa, uamuzi wake kutaka kujiondoa kwa kesi hiyo haukutokana na vitisho wala kulazimishwa na yeyote.