Connect with us

General News

Moto waua watu 5 wakiwemo jamaa 3 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Moto waua watu 5 wakiwemo jamaa 3 – Taifa Leo

Moto waua watu 5 wakiwemo jamaa 3

NA FARHIYA HUSSEIN

BIWI la simanzi limetanda katika mtaa wa Kibokoni, Kaunti ya Mombasa, baada ya watu watano kufariki, nyumba zao zilipoteketea Jumatano.

Miongoni mwa waliopoteza maisha yao katika moto huo uliotokea saa za asubuhi ni wanandoa wawili na mtoto wao.

Fatma Mohammed Abdalla, alikuwa akiendelea kuuza mahamri wakati mwendeshaji tuktuk alipomjulisha kwamba moto ulikuwa unateketeza nyumba yake ambayo ameishi kwa zaidi ya miaka 20.

Moto huo unashukiwa kuanzia katika nyumba ya jirani yake na kuenea hadi kwake.

“Nilianza kupiga kelele kuita majirani wasaidie kuokoa watu ambao walikuwa wako ndani ya nyumba. Mume, mkewe na mtoto wao ni miongoni mwa wale ambao walifariki. Mama alikuwa ameenda kujaribu kuokoa watoto wake. Alifanikiwa kuokoa mmoja ambaye amepata majeraha, lakini aliporudi kuokoa mwingine hakufanikiwa kutoka,” akaeleza Bi Mohammed.

Nyumba hiyo ya orofa mbili iliyojengwa kwa mbao iliteketea hadi kugeuka jivu.

Mkazi mwingine, Bw Adan Hussein, aliyepata majeraha mabaya ya moto kwenye mguu wa kulia alisema alisikia tu mlipuko mkubwa kabla ya huo moto kuanza.

“Nilikuwa ninatoka nje kuona ni nini kililipuka lakini nikakanyaga jivu moto ndipo nikapata majeraha,” akasema.

Katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Pwani, familia zilizoathirika zilikuwa na mshtuko jamaa wao wakijaribu kutafuta mahali ambapo wapendwa wao walikuwa wamelazwa.

Bw Mahmoud Ibrahim, alithibitisha kuwa waliofariki ni dadake, Bi Faiza Ali na mumewe, Jamal Ahmed pamoja na mtoto wao mmoja.

Alilaumu serikali ya Kaunti kwa kutochukua hatua za haraka kuepusha maafa na uharibifu uliotokea.

“Tunataka miili ya jamaa zetu ili tukafanye mazishi. Dadangu, Faiza alimwokoa mtoto wake mmoja ambaye pia alijeruhiwa akalazwa hospitalini. Alikuwa ameenda kumwokoa mtoto wa pili ndipo wote wakateketea,” akasema.

Mratibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya, Bw Mohammed Rajab, alisema watu watano walifariki papo hapo.

Wakazi wasiopungua watatu walisemekana kupata majeraha mabaya.

Bw Rajab alisema chanzo cha moto kilikuwa hakijabainishwa, kufikia wakati wa gazeti hili kuchapishwa.“Tulikimbiza wale waliojeruhiwa hadi hospitali za Pandya na Hospitali ya Rufaa ya Pwani,” akasema Bw Rajab.

Gari la idara ya zimamoto pamoja na ambulensi zilitatizika kufikia eneo la mkasa kutokana na changamoto za usafiri zilizoshuhudiwa katika siku ya kwanza ya utekelezaji wa mfumo mpya wa mweleko wa magari katikati ya jiji la Mombasa.

Hii ni kutokana na kuwa mpango huo ulisababisha misongamano katika baadhi ya barabara za mjini.

Kufikia wakati wa habari hii kuchapishwa, maafisa wa Serikali ya Kaunti ya Mombasa walikuwa hawajatoa taarifa kuhusiana na kisa hicho.

Viongozi mbalimbali wa kisiasa waliomboleza pamoja na jamaa waliopoteza wapendwa wao.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending