Connect with us

General News

Mvulana auawa na stima akiwa juu ya trekta – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mvulana auawa na stima akiwa juu ya trekta – Taifa Leo

Mvulana auawa na stima akiwa juu ya trekta

NA OSCAR KAKAI

MVULANA wa umri wa miaka 17 aliuawa na nyaya za stima kijijini Onoch eneo la Weiwei, Pokot Magharibi.

Daniel Chepkupe alikufa papo hapo alipopigwa na nyaya za stima zilizolewalewa kwenye barabara akiwa juu ya trekta ya kusafirisha vitunguu kutoka eneo la Kokotendwo likielekea katika soko la Ortum.

Kulingana na OCPD Sigor, Bamford Surwo, kijana huyo alikuwa kati ya wawili waliokuwa juu ya trekta iliyojaa magunia ya vitunguu.

“Kijana alikuwa amesimama juu ya trekta alipochapwa na nyaya za stima kwenye barabara hiyo. Mwenzake alijeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya misheni ya Ortum ambapo anaendelea kupokea matibabu,” akasema Bw Surwo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending