Connect with us

General News

ODM yaimarisha juhudi kupatanisha Nassir na Shahbal – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

ODM yaimarisha juhudi kupatanisha Nassir na Shahbal – Taifa Leo

ODM yaimarisha juhudi kupatanisha Nassir na Shahbal

Na BRIAN OCHARO

CHAMA cha ODM kiko mbioni kuepusha mpasuko ambao huenda ukatokea, iwapo mchujo wa kuamua atakayewania ugavana Kaunti ya Mombasa kwa tiketi ya chama hicho, hautaridhisha wanaotegea tiketi hiyo.

Kufikia sasa, ushindani mkali wa tiketi hiyo ni kati ya Mbunge wa Mvita, Bw Abdulswamad Nassir na mfanyabiashara, Bw Suleiman Shahbal.Naibu Gavana William Kingi, pia amepanga kuwania tiketi hiyo akitaka kurithi kiti cha Gavana Hassan Joho.

Mwenyekiti wa ODM tawi la Mombasa, Bw Mohamed Hamid, alithibitisha kuwa mashauriano bado yanaendelea kuona kama wanaotaka tiketi ya kuwania ugavana wanaweza kuelewana ili kusiwe na kura ya mchujo.

“Hayo mazungumzo hayajakamilika,” Bw Hamid alisema, alipoulizwa kuhusu suala hilo.Katika chaguzi zilizopita, baadhi ya wanasiasa waliokosa tiketi ya ODM waliamua kuwania kupitia kwa vyama tofauti au kama wagombeaji huru, wakafanikiwa kuwabwaga wagombeaji wa ODM katika maeneo tofauti yakiwemo ngome za chama hicho.

Ijapokuwa sheria za uchaguzi zilirekebishwa kwa njia inayolenga kuepusha tabia ya wanasiasa kuruka vyama wanaposhindwa katika mchujo, wadadisi wanasema vyama lazima viepuke uwezekano wa wanaoshindwa kuhamia kwingine.

Akizungumza na wanahabari katika afisi za chama hicho mtaani wa Ganjoni, Mombasa, Bw Hamid aliwataka wanasiasa wanaotafuta tiketi ya chama hicho, kuwania nyadhifa mbalimbali wakomeshe mizozano inayoweza kudhuru umoja wa chama hicho.

Aliwaomba wajitolee kukuza chama hata wanapojitafutia umaarufu kwa wananchi.“Ninaomba tushirikiane sote ili tuweze kuboresha chama chetu cha ODM. Tukishirikiana tutaweza kuinua chama juu zaidi ya vile ilivyo.

Ofisi hii ya ODM itafanya kazi na wawaniaji wote,” akasema Bw Hamid.Mwenyekiti huyo alikuwa akizungumza baada ya kukutana na Bw Shahbal aliyemtembelea katika afisi yake.Wito wake umetolewa wakati ambapo wanasiasa wanaotaka kuwania viti tofauti kupitia chama hicho mwaka ujao, wanaendeleza kampeni kabla ya kushiriki katika kura ya mchujo.

Kufikia sasa, baadhi ya wanachama wamejikusanya katika makundi tofauti kujipigia debe.“Uamuzi mwisho utatoka kwa wanachungwa wa Mombasa,” alisema akiongezea kuwa tayari chama hicho kimepokea majina ya zaidi ya watu 100 ambao wanataka kuwania kiti cha udiwani katika Kaunti ya Mombasa.

Bw Shahbal alisema alipendekeza kuwa matawi mengine ya chama hicho yafunguliwe Kaunti na maeneo mengine kama njia moja ya kukipa chama umaarufu zaidi.“Tumekubaliana kuwa matawi hayo yatafunguliwa na viongozi wa chama na hayatakuwa ya watu binafsi bali ya wanachama wote,” akasema.

Alikuwa ameandamana na mbunge wa zamani wa Kisauni, Bw Rashid Bedzimba.Viongozi hao walisema kuwa Mombasa bado ni ngome ya ODM na wakawarai wananchi wajitokeze kwa wingi na kujiandikisha kama wapiga kura ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi.

Bw Hamid alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Bw Mohammed Hatimy aliyefariki Novemba mwaka jana.