Raila aahidi kufagia mafisadi katika idara ya mahakama
NA COLLINS OMULLO
MWANIAJI wa kiti cha urais kupitia vuguvugu la Azimio la Umoja Raila Odinga amesema kuwa iwapo atashinda uchaguzi mkuu wa Agosti 9, atasafisha idara ya mahakama ili kuipa nguvu zaidi ya kupambana na vundo la ufisadi.
Bw Odinga alifafanua kuwa hatawasaza hata wanafamilia wake iwapo watapatikana wameshiriki ufisadi huku akisema kuna baadhi ya majaji na mawakili ambao wanatatiza mkondo wa haki kwenye idara ya mahakama.
Aliwarejea mawakili hao kama wanaotumia sheria kuwa mhusika hana hatia hadi idhibitishwe na mahakama kuwaachilia wafisadi ambao pia hutatiza kesi hizo na mwishowe mashahidi kujiondoa.
“Idara ya mahakama imekuwa ikiwaachilia washukiwa kwa dhamana na kesi zao huwa haziorodheshwi kusikizwa.
Kesi zilizowasilisha kortini mnamo 2018 bado hazijasikizwa. Kwa hivyo, ufisadi uliokolea katika idara ya mahakama pia umechangia kulemaza vita dhidi ya ufisadi,” akasema Bw Odinga aliyekuwa akizungumza katika jumba la Chatham mnamo Jumatano jioni.
Aidha Bw Odinga alikashifu asasi za uchunguzi akisema pia zimekosa kuwajibika vilivyo hasa katika kesi nyingi za ufisadi. Hasa alielekezea kidole cha lawama kwa Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) kwa kukosa kutekeleza wajibu wake vilivyo hata kwenye zile kesi ambazo wamepokezwa ushahidi.
Kutokana na hilo, washukiwa wengi wamekuwa wakiachiliwa huru huku kesi zao nazo zikijikokota kortini. Waziri huyo mkuu wa zamani aliahidi kuhakikisha anaisafisha idara ya mahakama kwa kuwa Wakenya wengi wameumia kutokana na kufeli kwa idara hiyo kupambana na ufisadi na mikon – do mingine ya haki.
“Tutahakikisha mchakato wetu wa kusafisha unaanza kwa afisa wa polisi anayechun – guza kesi hadi kwa idara ya mahakama ili asasi zote zinazojihusisha na vita dhidi ya ufisa – di ziwajibike vilivyo,” akasema.
Huku akisisitiza kuwa hakuna mfisadi atakayekwepa mkondo wa kisheria chini ya utawala wake, kiongozi huyo wa ODM alisikitika kuwa nchi hupoteza Sh700 bilioni kila mwaka kutokana na ufisadi.
“Iwapo unataka kupigana na ufisadi basi anza na wewe mwenyewe. Iwapo mwanafamilia wako amehusishwa na ufisadi, basi lazima sheria ifuatwe. Nitayafuate yale ambayo Rais Kagame alifanyia jamaa zake kule Rwanda,” akasisitiza.
Kiongozi huyo wa upinzani alimwondolea Rais Uhuru Kenyatta lawama kuhusiana na vita dhidi ya ufisadi akisema kuwa alikuwa ameshikwa mateka asipambana na uovu huo kwa kuwa juhudi zake zilikuwa zikitatizwa na Naibu Rais Dkt William Ruto.
“Rais mwenyewe alikiri hadharani kuwa serikali hupoteza Sh2 bilioni kila siku kutokana na ufisadi. Pia alikiri kuwa alikuwa anashindwa kukabili hali hiyo kwa sababu kila hatua ya kupigana na ufisadi ilikuwa ikiingizwa siasa, “Wakati mwanasiasa mfisadi anakamatwa na kufikishwa mahakamani, huwa kuna kilio kuwa jamii yake inalengwa kwa sababu inaegemea mirengo fulani ya kisiasa,” akasema.