Connect with us

General News

Ruto ageuka kiazi moto kwa Jubilee – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ruto ageuka kiazi moto kwa Jubilee – Taifa Leo

Ruto ageuka kiazi moto kwa Jubilee

Na WANDERI KAMAU

JUHUDI za baadhi ya wanasiasa wa chama cha Jubilee (JP) kumfurusha Naibu Rais William Ruto kutoka chama hicho zimegeuka kuwa kibarua kikubwa, kadri Uchaguzi Mkuu wa 2022 unavyokaribia.

Kwa muda sasa, maafisa wakuu katika chama hicho wamekuwa wakitishia “kumwadhibu” Dkt Ruto kwa madai ya kufanya kampeni za mapema na kumkosea heshima Rais Uhuru Kenyatta, japo hawajatimiza vitisho hivyo.

Kulingana na wadadisi, dalili ya kwanza ni hatua ya chama hicho kuahirisha ghafla Kongamano la Kitaifa la Wajumbe (NDC) lililopangiwa kufanyika mwishoni mwa Novemba.Ingawa haijabainika wazi wakati kongamano hilo litafanyika, duru zinasema limepangiwa kufanyika mwanzoni mwa Desemba.

Ingawa uongozi wa chama umekuwa ukikanusha uwepo wa juhudi za kumfurusha Dkt Ruto kama naibu kiongozi, duru ziliiambia ‘Taifa Leo’ kwamba, hiyo ilikuwa mojawapo ya ajenda kuu ya kongamano hilo.Baadhi ya waandani wa Rais Kenyatta wanadaiwa kueleza hofu kwamba, hatua ya kumfurusha Dkt Ruto chamani itakuwa “kosa kubwa la kisiasa” kwao.

“Ni kweli kuna hofu kuwa ni mapema mno kumwondoa Dkt Ruto. Miezi tisa kabla ya uchaguzi mkuu ni muda mrefu sana kufanya mageuzi kama hayo. Lazima tutahadhari,” akasema mbunge ambaye hakutaka kutajwa.

Wadadisi wanasema hatua nyingine inayoashiria hofu hiyo ni kutofaulu kwa vitisho vya baadhi ya wabunge wa Jubilee na chama cha Amani National Congress (ANC) kuwasilisha mswada wa kutokuwa na imani na Dkt Ruto katika Bunge la Kitaifa.

Mnamo Februari, Mbunge Ayub Savula (Lugari) alisema juhudi za kumng’oa mamlakani Dkt Ruto zilikuwa zimeshika kasi. Mbunge huyo, ambaye ndiye Naibu Kiongozi wa ANC na mshirika wa karibu wa kiongozi wa chama hicho, Musalia Mudavadi, alisema tayari alikuwa ashapata saini za wabunge 126 kutoka Jubilee kuunga mkono hoja hiyo.

Alisema alikuwa akizungumza na wabunge wengine 107 kutoka vyama vya mrengo wa NASA kumwezesha kufikisha idadi hiyo.Kisheria, hoja hiyo ilifaa kuungwa mkono na wabunge 233 ili kufaulu.Licha ya juhudi hizo, Katibu Mkuu wa Jubilee, Bw Raphael Tuju, alisema baadaye kwamba chama hicho hakikuwa na mipango yoyote ya kumfurusha Dkt Ruto kutoka wadhifa wake.

Tangu wakati huo, chama kilinyamazia suala hilo hadi sasa.Suala jingine linaloonekana kuilemea Jubilee ni tishio la kukiondoa chama cha UDA kama moja ya vyama tanzu vilivyounganishwa kubuni chama hicho 2017.

Awali, UDA ilijulikana kama Party of Development and Reform (PDR) kabla ya kubadilishwa jina na waandani wa Dkt Ruto.Dkt Ruto ametangaza atawania urais kupitia chama hicho, akiitaja Jubilee kama “chama kilichouliwa na watu wenye ubinafsi.

”Wakosoaji wa Dkt Ruto wamekuwa wakimlaumu kwa “kutwaa kwa nguvu chama ambacho hakukitengeneza na hukitumia kuishanmbulia serikali.”Baadhi ya wanasiasa walioapa kuendesha mchakato huo ni Naibu Mwenyeiti wa Jubilee David Murathe na mbunge Jeremiah Kioni (Ndaragwa).

“Haya ni kama mapinduzi ndani ya chama. Ikiwa (Ruto) anataka kuendelea na kampeni zake, basi atangaze kuondoa UDA kuwa miongoni mwa vyama washirika wa Jubilee ama tumwondoe sisi wenyewe,” akatishia Bw Murathe.Hadi sasa, uongozi wa Jubilee haujawahi kutekeleza vitisho hivyo.