Connect with us

General News

Ruto alaani mswada wa mageuzi ya sheria ya uchaguzi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ruto alaani mswada wa mageuzi ya sheria ya uchaguzi – Taifa Leo

Ruto alaani mswada wa mageuzi ya sheria ya uchaguzi

Na CHARLES WASONGA

NAIBU Rais William Ruto amepinga mswada unaolenga kupiga marufuku upeperushaji wa matokeo ya uchaguzi moja kwa moja pindi yanapotangazwa katika vituo vilivyoko katika maeneobunge kote nchini.

Kwenye taarifa fupi kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter, Alhamisi, Februari 3, 2022, aliwashutumu wadhamini wa mswada huo akidai lengo lao ni kuiba kura katika uchaguzi mkuu ujao.

Dkt Ruto alisema maafisa wa cheo cha juu serikalini wanalenga kuwalazimishia Wakenya “kikaragosi” wao ili awe rais wao, kupitia marekebisho ya sheria ya uchaguzi.

Naibu Rais alitaja njama hiyo kama haramu, yenye malengo maovu na ambayo itafeli.

“Mswada huu wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi umeletwa kwa lengo la kuvugu demokrasia na uhuru wa Wakenya kuchagua rais wao. Njama hiyo ni mbovu na itafeli. Wakenya wamekataa kuelekezwa na kupangwa,” Dkt Ruto akasema.

Naibu Rais alimsuta Rais Uhuru Kenyatta na wandani wake kwa kujaribu kuwahakikishia kuwa Raila Odinga anatangazwa mshindi katika uchaguzi mkuu ujao, “kupitia sheria mbovu.”

Akaongeza: “Hii njia ya kuvuruga katiba kupitia mabadiliko ya sheria muhimu ni sawa na mapinduzi – inatisha uhuru wa watu wa Kenya.”

Mswada huo wa marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi, 2022, umedhaminiwa na kiongozi wa wengi katika Bunge la Kitaifa Amos Kimunya.

Mswada huo unalenga kuifanyia marekebisho sheria ili kutoka kwa uwasilishaji wa matokeo ya uchaguzi wa urais kielektroniki na kupitia uwasilishaji wa fomu za matokeo.

Chini ya sheria ya sasa, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inahitajika kuweka miundomsingi ya kuwezesha uwasilishaji wa matokeo ya urais kielektroniki pekee.

Matokeo hayo hutangazwa na maafisa wa usimamizi katika vituo vya upigaji kura na pia hupeperushwa moja kwa moja.

Chini ya sheria ya sasa Wakenya wameweka kujumuisha kura za wagombeaji urais wanaowataka moja kwa moja yanavyopeperushwa kupitia runinga na kupitia mitandao mingine.

Vile vile, IEBC inaweza kutumia matokeo yaliyotangazwa katika vituo vya kupigia kura na kuwasilishwa kieletroniki hadi kituo cha kitaifa cha kujumuisha kura jijini Nairobi.

Lakini kwa mujibu wa mswada huu, maafisa wa kusimamia vituo vya kupigia kura, wataweza kupiga picha fumo za matokeo na kuzituma katika kituo cha kitaifa cha kujumuisha matokeo ya kura za urais.

Maafisa hao pia wanahitajika kuwasilisha fomu hizo za matokeo moja kwa moja kwa kusafiri hadi katika kituo cha eneo bunge.

Baadaye afisa msimamizi wa uchaguzi katika eneo bunge atajumuisha matokeo kutoka vituo vyote na kuyawasilisha katika kituo cha kitaifa cha kujumuisha kura, Nairobi.

“Msimamizi wa uchaguzi katika eneobunge atajumuisha matokeo katika fumo rasmi, (Form 34B) na kuwasilisha matokeo hayo yeye binafsi hadi kituo cha kitaifa cha kujumuisha matokeo pamoja na fomu hitajika,” mswada huo unasema.

Mswada huo pia unamlazimisha mwenyekiti wa IEBC kutangaza tu matokeo rasmi baada ya kupokea matokeo yote ya urais kutoka maeneo bunge yote 290.

Sheria ya sasa inatoa nafasi kwa mwenyekiti wa IEBC kutangaza mshindi wa uchaguzi wa urais ikiwa matokeo kutoka maeneobunge yaliyosalia hayaathiri matokeo ya mwisho.

Msukumo wa kufanyiwa mageuzi kwa sheria ya uchaguzi unajiri siku chache baada ya wabunge wafuasi wa Dkt Ruto na wale wa Rais Uhuru Kenyatta na Bw Odinga, kukwaruzana kuhusu mswada tata wa mageuzi ya sheria za vyama vya kisiasa.

Hata hivyo, mswada huo ulipitishwa licha ya pingamizi kutoka kwa wandani wa Dkt Ruto.