Connect with us

General News

TUSIJE TUKASAHAU – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

TUSIJE TUKASAHAU – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU

KUNA hofu kwamba bei ya unga wa mahindi itapanda zaidi kufuatia hatua ya Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB) kuongeza bei ya kununua zao hili kutoka kwa wakulima kutoka Sh2,700 hadi Sh3,000 kwa gunia moja la kilo 90.

Hii ina maana kuwa kampuni za kusaga unga wa mahindi zitalazimika kununua mahindi kwa bei ya juu, hali itakayochangia kuongezeka kwa bei ya unga kwa zaidi ya bei ya sasa ya Sh120 kwa pakiti ya kilo mbili madukani.

Lakini Waziri wa Kilimo, Bw Peter Munya (pichani) anafaa kufahamu kwamba anaweza kuwakinga Wakenya kutokana na ongezeko la bei ya unga kwa kuingilia kati na kuhakikisha kuwa kampuni za kusaga unga zinauziwa mahindi kwa bei nafuu.

Bw Munya asije akasahau kwamba mnamo 2018, mtangulizi wake, Mwangi Kiunjuri, aliamuru NCPB ipewe ruzuku ya Sh6 bilioni kutoka kwa Hazina ya Kitaifa kuiwezesha kupunguza bei ya mahindi kwa kampuni za kusaga unga.

Hatua hiyo ilichangia kushuka kwa bei ya unga kutoka Sh150 hadi Sh75 kwa pakiti ya kilo mbili.