Connect with us

General News

Wa Iria asema hatabadilisha nia kuwania urais 2022 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wa Iria asema hatabadilisha nia kuwania urais 2022 – Taifa Leo

Wa Iria asema hatabadilisha nia kuwania urais 2022

Na KENYA NEWS AGENCY

GAVANA Mwangi wa Iria wa Murang’a amesisitiza kuwa hatabadilisha nia yake kuwania urais 2022.

Bw Wa Iria pia alisisitiza kwamba hatakuwa mgombea-mwenza wa mwaniaji yeyote wa urais.Jumatatu, gavana huyo alisema anawawakilisha wenyeji wa Mlima Kenya, hivyo wawaniaji wengine wako huru kujiunga naye kubuni serikali ijayo.

“Siwezi kuwa mgombea-mwenza wa kigogo yeyote. Badala yake, ninatafuta uungwaji mkono kutoka kwa wawaniaji kama kiongozi wa ODM, Raila Odinga, Musalia Mudavadi (ANC) kati ya wengine. Wanapaswa kuniunga mkono ili tuweze kubuni serikali ijayo,” akasema Bw Wa Iria, alipokutana na wenyeji katika Uwanja wa Ihura.

Alisema atawarai wapigakura kutoka eneo la Kati kuunga mkono azma yake, ikizingatiwa kuwa kila mmoja yuko huru kuwania nafasi yoyote ikiwa ametimiza viwango vinavyotakikana. “Hatupaswi kuambiwa eneo la Mlima Kenya halipaswi kuwa na mgombea urais wakati huu. Katiba i wazi. Hakuna eneo linalozuiwa kuwa na mgombea urais mwaka ujao,” akasema.

Gavana huyo anahudumu kwa muhula wa pili, na ni miongoni mwa viongozi kadhaa kutoka eneo hilo ambao wametangaza nia ya kuwania urais mwaka ujao.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending