Connect with us

General News

Wito wahariri waongeze makala ya filamu za Kenya Wikipedia – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wito wahariri waongeze makala ya filamu za Kenya Wikipedia – Taifa Leo

Wito wahariri waongeze makala ya filamu za Kenya Wikipedia

Na WANGU KANURI

MTANDAO  wa taarifa kuhusu watu mashuhuri, maeneo na dhana za kidunia Wikipedia sasa umeimarisha ushirikiano wake na Tume ya Filamu nchini (KFC) ili kuwapa wahariri dondoo na marejeleo ya uigizaji ambayo wamekuwa wakikosa.

Makala ya Wikipedia yatasaidia kuhifadhi data kuhusu sekta ya uigizaji nchini, kwa kuhakikisha kuwa taarifa zinazochapishwa ni halisi, za kweli na hazina mapendeleo.

Akizungumza katika mkutano wa Wikimedia uliofanyika katika hoteli ya Weston jijini Nairobi Bi Winnie Kabintie, mhariri wa Wikipedia na afisa wa mradi wa Afrocine alisema wakati umefika kwa sekta ya filamu nchini kupigiwa debe kupitia Wikipedia.

Aliwarai wahariri wa humu nchini kushiriki katika mradi huo ambao unalenga kuhakikisha kuwa kila mwigizaji maarufu ametengenezewa ukurasa wake kwenye Wikipedia.

“Wahariri huhakikisha kuwa wanachochapisha ni kuhusu mtu mashuhuri na taarifa wanayochapisha imezungumziwa na vyombo tajika vya habari.” akaongeza Bi Kabintie.

Licha ya dhana kuwa Wikipedia huandika wasifu wa watu mashuhuri, uandishi wao huangazia yote kumhusu mtu huyo bila kuegemea uzuri wake pekee, Bi Kabintie alisema watatumia makala na habari zilizochapishwa katika vyombo vya habari nchini kuhakikisha taarifa zote ni sahihi.

Vilevile, matapeli wanaovuna wasipopanda katika sekta ya filamu sasa watazimwa baada ya KFC kuidhinisha mchakato wa kuunda kadi spesheli zitakazowatambua waundaji filamu halali.

Bi Grace Kago, mkuu wa makuzi ya hadhira katika KFC alieleza kuwa mradi huo utakaoanza 2022 utawasaidia waigizaji kuwatambua waundaji filamu ghushi.

Alisema KFC imenuia kuanzisha duka la mtandaoni la filamu la E-Film litakalowawezesha waundaji filamu kupata maeneo na vifaa watakavyohitaji kurekodi filamu zao nchini na hata nje ya nchi.

“E-Film itawasaidia waundaji filamu kupata maarifa kuhusu uundaji wa filamu na sheria wanazopaswa kuzingatia,” akaongezea Bi Kago.

Aidha ili kuwepo na data za filamu nchini, KFC ilianzisha Akaunti ya Setilaiti ya Utengenezaji wa Filamu na tayari imekusanya data kutoka 2019.

“Kumekuwa na uhaba wa ujumbe kuhusiana na filamu jambo ambalo limechangia ukosefu wa data,” akasema Bi Kago.

Baada ya ukusanyaji wa data, KFC imesema itajenga wasifu wa waigizaji nchini, itatathmini mchango wa tume kwenye uchumi wa Kenya na hata kujua mapato yanayoletwa na utengenezaji filamu.

Bi Winnie Kabintie (kushoto) na Bi Grace Kago baada ya kikao cha kuhamasisha waandishi kuhusu filamu za humu nchini katika Hoteli ya Weston, Nairobi. Picha/ Faustine Ngila

Kulingana na Bi Kabintie, viongozi nchini Afrika wanapaswa kuhakikisha kuwa mikakati wanayoweka hairudishi nchi nyuma haswa kidijitali.

Mwanzilishi wa mradi wa Afrocine, Sam Oyele akizungumza kupitia mtandao wa Zoom kutoka Nigeria aliwarai wahariri wa Wikipedia kuongeza makala kuhusu waigizaji na wanaochangia kwenye filamu nchini Kenya.

Faith Munyolo, mmoja wa washiriki wa kamati ya Wikimedia nchini Kenya alishabikia utumizi wa picha kueleza kuhusu masuala mbalimbali.

Kwa mfano kwenye shindano la Wiki Loves Earth, liliofanywa kwa mara ya tisa mwaka huu, washindani waliweza kupiga picha za malighafi yaliyomo kwenye nchi zao.

Washindi kutoka nchi mbalimbali waliweza kupewa tuzo huku mshindani mmoja akipewa udhamini wa kuhudhuria Wikimania (Mikutano ya kila mwaka ya Wikimedia) ama vocha ya Amazon iliyo na thamani sawa.

“Kupitia miradi ya shindano za picha, Wikipedia inachangia uenezi wa maarifa bila malipo kwa watu uliwenguni,” akaeleza.

 

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending