Connect with us

General News

Wabunge wa Ruto katika njiapanda – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wabunge wa Ruto katika njiapanda – Taifa Leo

Wabunge wa Ruto katika njiapanda

LEONARD ONYANGO NA RICHARD MUNGUTI

SHERIA mpya ya Vyama vya Kisiasa imeanza kuwatia wasiwasi wabunge wa Jubilee wanaolenga kuhamia chama cha United Democratic Alliance (UDA) kinachoongozwa na Naibu Rais William Ruto.

Kulingana na Msajili wa Vyama vya Kisiasa Ann Nderitu, wabunge wanaolenga kuhama vyama walivyotumia 2017, watahitajika kuandika barua kwa Karani wa Bunge na chama kilichowafadhili kabla ya kuidhinishwa kujiunga na vyama vipya.

Wakili wa Masuala ya Sheria na Katiba, Jackson Awele anasema kwa mujibu wa sheria hiyo mpya, wabunge, maseneta na madiwani wanaohamia vyama vingine wanajitia katika hatari ya kupoteza viti vyao.

Wabunge zaidi ya 100 wa Jubilee walikuwa wametishia kuhamia rasmi UDA kufikia Feb – ruari 8, mwaka huu, lakini wakabadili nia.

Kulingana na sheria hiyo mp – ya, siku ya mwisho kwa wanasiasa kujiunga na vyama vipya itakuwa Machi 26, mwaka huu.

“Sheria hiyo mpya inahitaji kwamba sajili ya wanachama wa vyama vya kisiasa ziwasilishwe kwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa kuidhinishwa siku 14 kabla ya kupelekwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Tume ya IEBC ni sharti ikabidhiwe sajili hizo miezi mitatu kabla ya Uchaguzi Mkuu,” anaeleza Bw Awele.

Hiyo inamaanisha kuwa, kwa mfano, wandani wa Dkt Ruto watakaokosa kuhamia UDA kufikia Machi 26 hawataruhusiwa kuwania nyadhifa kwa kutumia chama hicho.

Bw Owele anasema kuwa hatima ya wabunge watakaohamia UDA itakuwa mikononi mwa Jubilee.

“Jubilee watatumia barua zilizoandikiwa Karani wa Bunge kama ushahidi na kuwasilisha ombi kwa Spika wa Bunge kutaka viti vyao vitangazwe kuwa wazi,” Bw Awele akaambia Taifa Leo.

Kulingana na Kifungu cha 103 (e) cha Katiba, mbunge anayegura chama alichotumia kuingia Bungeni anapoteza kiti chake.

Wakili John Khaminwa aliambia Taifa Leo kuwa Katiba inahitaji kuwa wabunge wanao – hamia vyama vingine wajiuzulu hivyo wanastahili kufanya hivyo bila kukimbilia kortini ili kuendelea kupokea mshahara wa miezi minne iliyosalia.

Lakini Katibu Mkuu wa Jubilee Raphael Tuju alisema kuwa viti vya wabunge watakao – hamia UDA vinafaa kutangazwa kuwa wazi. Lakini anasema kuwa wabunge hao huenda wakaenda mahakamani kupinga hivyo

kupoteza muda mwingi kupinga.

Wakili wa masuala ya Katiba Bobby Mkangi pia anasema kuwa viti vya wabunge wanaogura vyama vyao vinafaa kusalia wazi.

“Litakuwa jukumu la chama husika cha kisiasa kutumia njia zote ikiwemo kwenda mahakamani kuhakikisha kuwa wabunge waliohama wanaachana na viti vyao Bungeni,” anasema.

Mswada wa Kufanyia Marekebisho ulipingwa vikali na wandani wa Dkt Ruto katika Bunge la Kitaifa lakini ukapitishwa bila pingamizi katika Seneti.

Wandani wa Dkt Ruto waliozungumza na Taifa Leo, walisema kuwa wanasiasa wa UDA wanaendelea kufanya mashauriano na mawakili kabla ya kuhama rasmi kutoka Jubilee.

Wanasiasa wa UDA iwapo watahama Jubilee na mahakama iseme kwamba wanafaa kuondoka afisini, watatoa mwan – ya kwa wenzao wa Azimio la Umoja kupitisha miswada zenye utata kama vile Mswada wa Huduma Namba.

Mswada huo unapendekeza IEBC itengeneze daftari la wapigakura kutoka kwa mfumo wa Huduma Namba (NIIMS). Pendekezo hilo limepingwa vikali na wandani wa Dkt Ruto kuwa ni njama ya kuipa kura kumpendelea kinara wa Azimio la Umoja Raila Odinga.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending