Connect with us

General News

Wakulima walia hasara kwa kukosa soko la matunda – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakulima walia hasara kwa kukosa soko la matunda – Taifa Leo

Wakulima walia hasara kwa kukosa soko la matunda

NA SIAGO CECE

BAADHI ya wakulima wa matunda katika Kaunti ya Kwale, wanapata hasara kutokana na ukosefu wa soko kwa bidhaa zao licha ya mavuno mengi.

Wakulima katika Wadi ya Kubo Kusini, wanasema matunda yao mengi yanaharibika katika mashamba yao, huku wakinyanyaswa na mawakala.

Bi Sabina Jeremiah, 73, alisema ingawa amepata mavuno mengi, hana wanunuzi.