Connect with us

General News

Watoto walemavu zaidi ya 200 Mukuru wapigwa jeki kielimu baada ya Kenya Child Foundation Ireland kuwajengea kituo cha kisasa cha kusomea na kufanyiwa mazoezi ya viungo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Watoto walemavu zaidi ya 200 Mukuru wapigwa jeki kielimu baada ya Kenya Child Foundation Ireland kuwajengea kituo cha kisasa cha kusomea na kufanyiwa mazoezi ya viungo – Taifa Leo

Watoto walemavu zaidi ya 200 Mukuru wapigwa jeki kielimu baada ya Kenya Child Foundation Ireland kuwajengea kituo cha kisasa cha kusomea na kufanyiwa mazoezi ya viungo

Na SAMMY KIMATU

NAIROBI

WATOTO walemavu zaidi ya 200 katika maeneo ya Mukuru wamepigwa jeki kielimu na wafadhili kutoka nchini Ireland baada ya kujengewa jumba la kisasa lililo na madarasa na vyumba vya kufanyia mazoezi ya viungo.

Jumba hilo limejengwa ndani ya kituo cha Songa Mbele na Masomo kilicho katika mtaa wa mabanda wa Mukuru-Kisii, kaunti ndogo ya Starehe.Wafadhili hao,The Kenya Child Foundation-Ireland (KCF-I), pia waliahidi kutoa msaada wa vifaa, kuanzisha mradi wa kupanda miti, nyasi na maua ili kuboresha   mazingira ya kituo hicho.

Ujumbe wa KCF-I uliongozwa na mwenyekiti wao, Bw John McCarrick akiambatana na wakurugenzi wa bodi Bi Ciara McCarrick, Bw Gerand Kelly na Bi Hellen Kelly. Wageni hao walipokelewa na mkurugenzi Mkuu wa Mukuru Promotion Centre (MPC) mtawa Mary Killeen na Mshirikishi wa Songa Mbele, Mtawa Mary Akinyi.

Kituo cha Songa Mbele husimamiwa na MPC.

“Nia yetu ni kuwasaidiA watoto walemavu kupata elimu kwani ni haki yao kusomeshwa licha ya changamoto wanazopitia ikiwemo maumbile yao ya kuzaliwa,magonjwa na ajali,” Bw Carrick asema. Vilevile, mtawa Killeen aliwapongeza wafadhili hao na kuongeza kwamba elimu kwa watoto walemavu ni changamoto kwa wazazi waliolemazwa na umaskini katika jamii.

“Japo ni lazima kila mtoto kupata elimu hapa nchini Kenya, ni changamoto kubwa kwa wazazi maskini katika mitaa ya mabanda hapa Mukuru unaochangiwa na ukosefu wa ajira kabla na pia bwakati janga la Corona iliripotiwa nchini,” Mtawa Killeen akanena.

Fauka ya hayo, Mtawa Killeen aliambia Taifa Leo kwamba walemavu wa maskio hawana vifaa vya kuwawezesha kusikia akitaja kwamba ni ghali mno kununulika madukani na masokoni. Vilevile, alisema walimu wa watoto walio na mahitaji spesheni ni wachache ikilinganishwa na viwango vya Umoja wa Mataifa vya uwiano (ratio) ya mwalimu mmoja kwa wanafunzi watano.

“Kinyume na uwiano wa mwalimu mmoja kuwa na watoto watano, hapa kwetu ni mwalimu mmoja kwa watoto 16,” Mtawa Killeen asema. Mshirikishi wa Songa Mbele, Mtawa Akinyi aliongeza kwamba wanafunzi hutatizika sana wanapomaliza kusoma au kufanyiwa mazoezi ya viungo.

Aliambia wanahabari kuwa ni mzigo kwa wazazi kwani wazazi huwa hawana vifaa vya kuwabebea wanao na badala yake hulazimika kuwabeba mgongoni hadi makwao na kuwaleta asubuhi kwa usafiri huo. “Kumbeba mtoto kutoka nyumbani hadi shuleni kwa mgongo na vilevile kutoka shuleni kurudi nyumbani ni mzigo kwa mzazi,’’ Bi Akinyi asema.

Alisema fauka ya kuwa na kituo cha Songa Mbele mtaani karibu na maskani ya wanafunzi wake, kuna watoto wengine wa kituo hicho husomea vituoni vingine badala vya malazi au vilivyo na mabweni. Hii ni kwa sababu kituo cha Songa Mbele kina uhaba wa vifaa vya kukimu mahitaji ya mtoto mlemavu kutoka mmoja hadi mwingine ndiposa wanasomea vituoni vingine.

“Kuna wale watoto wetu wanaosomea katika mji wa Thika na jijini Nairobi-kaunti ndogo ya Kasarani vilivyo katika kaunti ya Kiambu na Nairobi mtawalia,” Bi Akinyi akaongeza. Wageni walitumbuizwa na watoto na walimu kwa densi na nyimbo, wakala mankuli ya mchana pamoja na kutangamana kabla ya hafla kumalizika.

Hata hivyo, waliahidi kuwa watakuwa wakiwatembelea kila mwezi wa Julai kila mwaka na kuzidi kuwapatia watoto msaada wowote wa kuwafaa kielimu kutoka kwao binafsi sawia na marafiki wao. KCF pia imejenga shule ya umma kwa jina St Patrick’s katika eneo la Kibwezi katika kaunti ya Makueni.

“Tulianzisha shule ya St Patrick’s mwaka 2015 ikiwa na madarasa tatu na wanafunzi 30. Leo tuna watoto 250, darasa 11 na walimu 11. Shule limeanzia Gredi 1 hadi darasa la Nane,” Bw Mc Carrick akasema.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending