Utafiti ulionesha kuwa maski zinapunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kuambukizwa coronavirus endapo utagusana na mwathiriwa. Source: Depositphotos
Kulingana na ripoti ya Citizen Digital walifikishwa katika mahakama ya Rongo ambapo walitozwa faini ya KSh 1,000 kila mmoja.
Kwa siku tatu zilizopita, idadi ya watu 47 wamekamatwa na kutozwa faini ya kati ya KSh 1,000 na KSh 5,000 eneo bunge la Rongo kwa kutovalia maski wakiwa kwa umma.
Eneo la Suna Mashariki, msako sawia na huo unaendelezwa na maafisa wa afya wakishirikiana na wale wa usalama.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema ni lazima kila mmoja avalie kitavua akiwa maeneo ya umma au kwenye gari liwe la umma au la binafsi. Picha: MoH. Source: UGC
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema ni lazima kila mmoja avalie kitamvua akiwa maeneo ya umma au kwenye gari liwe la umma au la binafsi.
Alichapisha kanuni katika gazeti la kitaifa akitaja faini ambayo mtu atatozwa akipatikana akikiuka sheria hizo ambapo huenda akalipa faini ya KSh 20,000 au kufungwa kwa miezi sita.
Utafiti ulionesha kuwa maski zinapunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kuambukizwa coronavirus endapo utagusana na mwathiriwa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.