Mwanahabari wa runinga ya NTV Kennedy Muriithi Jumatano,Juni 17, alijipata pabaya alipokuwa akifuatilia taarifa kuhusu vyama vya CCM na Wiper kujiunga na Jubilee.
Muriithi alikuwa na wenzake katika makao makuu ya chama cha Jubilee alipomuuliza kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka swali kuhusiana na hatua ya chama chake.
Kalonzo Musyoka aliwahi kumpuuza ripota Kennedy Muriithi na kumwambia jina lake linamsaliti. Picha: NASA Source: UGC
Kwenye hafla hiyo, Wiper na CCM vilitia sahihi mkataba wa kufanya kazi pamoja na chama cha Jubilee kwenye bunge na seneti.
Si mara ya kwanza kwa Muriithi kujipata pabaya kwani wakati ambapo siasa za NASA zilikuwa zimeshika moto 2017, Kalonzo alimpuuza na kusema swali lake lilifanana na jina lake.
“Jina lako linakusaliti,” Kalonzo alimwambia wakati huo baada ya kuulizwa swali.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690